Pata taarifa kuu

Ndege isiyo na rubani ya jeshi la Niger yaua raia kimakosa

Shambulio la ndege isiyo na rubani ya jeshi la Nigeria limewaua kimakosa na kuwajeruhi raia waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya kidini ya Kiislamu katika kijiji cha kaskazini-magharibi, mamlaka za ndani, jeshi na mkazi mmoja wamesema siku ya Jumatatu.

(picha ya kielelezo)
(picha ya kielelezo) © AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi mara nyingi hutumia mashambulizi ya angani kupambana na makundi ya majambazi na waasi wa kijihadi wanaoendesha harakati zao kwa miaka 14 kaskazini mashariki na kaskazini magharibi mwa nchi. Hadi sasa serikali haijatoa ripoti ya shambulio hili la bomu lililotekelezwa katika jimbo la Kaduna, lakini mkazi wa kijiji kilichoathiriwa amesema kuwa shambulio hilo liliua watu 30 siku ya Jumapili jioni.

"Waumini wa Kiislamu waliokuwa wakisherehekea Maulid (sherehe za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad, SAW) waliuawa kimakosa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani iliyolenga magaidi na majambazi," amesema Gavana wa Jimbo la Kaduna, Bw. Uba Sani.

Wengi wa wahanga walikuwa wanawake na watoto, mkazi, Hassan Ma'aruf, ameliambia shirika la habari la  AFP kwa njia ya simu, ambaye alishiriki picha zinazoonyesha, kulingana naye, miili ya wanawake na watoto. Shirika la habari la AFP halikuweza kuthibitisha mara moja uhalisi wa picha hizo.

Makumi ya watu waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini huko Kaduna, kamishna wa usalama wa serikali Samuel Aruwan amesema katika taarifa, na kuthibitisha kuwa wengine kadhaa wameuawa. Amesema jeshi lilisema "liliwapiga bila kukusudia watu wa jamii" wakati likitekeleza misheni ya kawaida dhidi ya waasi.

"Sikukuu ya Maulidi ilikuwa ikifanyika kijijini hapo jana usiku ambapo mkusanyiko huo ulilipuliwa kwa bomu mwendo wa saa 9 alasiri. Hakuna aliyetarajia janga la aina hiyo. Hadi sasa tumegundua wahanga 30 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto", alisema mkazi wa kijiji hicho Hassan Ma'aruf.

Makundi ya magenge na majambazi yamekuwa yakisumbua sehemu za kaskazini-magharibi mwa Nigeria kwa miaka kadhaa, yakifanya uvamizi kwenye vijiji ili kuwateka nyara wakaazi ili wapate fidia. Wanafanya kazi kutoka kwa kambi katika misitu inayozunguka majimbo ya kaskazini-magharibi.

Kwa upande wao wanajihadi wanaendelea na vita vyao kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Kwa jumla, mzozo huo umesababisha zaidi ya watu 40,000 na milioni 2 kukimbia makazi yao tangu mwaka wa 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.