Pata taarifa kuu

Burkina na Niger wajiondoa katika Kikosi cha G5 Sahel

Burkina Faso na Niger, nchi mbili zinazoongozwa na majeshi yaliyonyakuwa madaraka kupitia mapinduzi, zimetangaza siku ya Jumamosi kwamba zimejiondoa katika kikosi cha G5 Sahel kinachopambana dhidi ya wanajihadi, zikijiungana na jirani yao Mali, iliyojiondoa katika kikosi hiki mwezi Mei 2022.

Nchi tano za G5 Sahel ziliunda jumuiya hii mnamo mwaka 2014 na kisha kuzindua jeshi lake mnamo mwaka 2017 wakati wanajihadi walikuwa wakiimarisha ngome zao katika nchi hizi, zenye majeshi yenye vifaa vya kutosha.
Nchi tano za G5 Sahel ziliunda jumuiya hii mnamo mwaka 2014 na kisha kuzindua jeshi lake mnamo mwaka 2017 wakati wanajihadi walikuwa wakiimarisha ngome zao katika nchi hizi, zenye majeshi yenye vifaa vya kutosha. 法廣 © RFI/Olivier Fourt
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili "zimeamua kwa uhuru wote kujiondoa katika taasisi zote za G5 Sahel, pamoja na Kikosi cha Pamoja", kuanzia Novemba 29, zimesema katika taarifa.

Jumuiya hii iliyoundwa mnamo mwaka 2014 kupambana dhidi ya wanajihadi katika ukanda wa Sahel, ilikuwa inaundwa na Mali, Burkina, Niger, Mauritania na Chad.

"Jumuiya hii imeshindwa kufikia malengo yake. Mbaya zaidi, matarajio halali ya mataifa yetu, kufanya nafasi ya G5 Sahel kuwa eneo la usalama na maendeleo limezuiliwa na uzani wa kitaasisi, nguvu ya kizazi kingine ambacho kinatushawishi kuwa njia ya uhuru na hadhi ambayo tunashiriki leo, ni kinyume na kushiriki katika G5 Sahel katika hali yake ya sasa ", Ouagadougou na Niamey wamebaini.

"G5 Sahel haiwezi kutumikia masilahi ya kigeni kwa uharibifu wa maslahi ya watu wa Sahel, hata chini ya kukubali udikteta kutoka nchi kadhaa zeny nguvu duniani kwa niaba ya ushirika uliopotoka na wa kitoto ambao wanakanusha haki ya uhuru wa watu wetu na kutoka Mataifa yetu, "nchi hizo mbili zimeongeza,na kudai kuwa zimechukua" jukumu la kihistoria "kwa kujiondoa kwenye jumuiya hiyo.

Mnamo mwezi Mei 2022, Mali, pia inayoongozwa na jeshi tangu mwaka 2020, ilijiondoa katika G5 Sahel, ikitaja kuwa jumuiya hiyo" inatumiwa na nchi za kigeni".

Nchi tano za G5 Sahel ziliunda jumuiya hii mnamo mwaka 2014 na kisha kuzindua jeshi lake mnamo mwaka 2017 wakati wanajihadi walikuwa wakiimarisha ngome zao katika nchi hizi, zenye majeshi yenye vifaa vya kutosha. Chad na Mauritania sasa ni washiriki wa jumuiya hii ambayo inaonekana kutoweka.

Serikali za kijeshi za Mali, Niger na Burkina, nchi tatu zinazokabiliwa na ghasia za wanajihadi na ambazo uhusiano wake na Ufaransa umedorora, zilikutana katika wiki za hivi karibuni kuunda muungano wa nchi za Sahel.

Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi hizi tatu walipendekeza siku ya Ijumaa jioni kuundwa kwa jumuiya, pamoja na matarajio ya kufikia shirikisho.

Burkina Faso ilikumbwa na mapinduzi mawili ya kijeshi mnamo mwaka 2022, wakati Niger inatawaliwa na majenerali ambao walichukua madaraka kwa nguvu mnamo mwezi Julai 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.