Pata taarifa kuu

UNDP: Ni kazi, sio itikadi za dini zinazovutia watu kujiunga na Wanajihadi

Ripoti mpya ya umoja wa mataifa inaonesha kuwa, itikadi za kidini sio kitu pekee kinachofanya raia barani Afrika kujiunga kwenye makundi ya kijihadi na makundi mengine yenye silaha.

Wapiganaji wa Al-Shabaab wakionesha silaha zao wakati wa moja ya mazoezi yao ya kijeshi kaskazini mwa Mogadishu, Somalia. 21 10 2010.
Wapiganaji wa Al-Shabaab wakionesha silaha zao wakati wa moja ya mazoezi yao ya kijeshi kaskazini mwa Mogadishu, Somalia. 21 10 2010. ASSOCIATED PRESS - Mohamed Sheikh Nor
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, umasikini na matamanio ya kupata ujira unaolipa vizuri ndio imekuwa kichocheo kikubwa cha vijana kujiunga na makundi ya wapiganaji.

Kwa hitimisho hili, kunaondoa kabisa dhana ya kuwa wengi ya watu waliojiunga na makundi ya kijihadi kama vile Boko Haram, Al Shabaab, Islamic State na Al Qaeda, ni kwasababi ya itikadi za kidini.

Wanajeshi wa Syria kwenye mji wa Hama
Wanajeshi wa Syria kwenye mji wa Hama AP - Alexander Kots
Mwaka 2021 shirika la umoja wa mataifa la mpango wa maendeleo UNDP, liliwahoji watu zaidi ya 2,000, katika mataifa nane, ikiwemo Burkina Faso, Cameroon, Chad, Mali, Niger, Nigeria, Somalia na Sudan.

Mahojiano yalijumuisha wapiganaji wa zamani zaidi ya 1,200, ambao kati yao 900 walijiunga kwa kupenda huku wengine walirubuniwa au kulazimishwa.

Miongoni mwa wale waliojiunga kwa kupenda, walisema kilichowavutia ni matamanio ya kulipwa vizuri, suala ambalo ndio lilikuwa msingi wa awali, imesema ripoti ya UNDP.

Hii inaonesha ongezeko la asilimia 92 la majibu yaliyotolewa, ukilinganisha nay ale yaliyotolewa mwaka 2017.

Katika nchi nyingi, kukosekana kwa kipato, fursa za ajira, maisha bora na msongo wa mawazo, vinawalazimisha watu kuchukua fursa yoyote ambayo watapewa. Amesema mkurugenzi wa UNDP, Achim Steiner.

Wengine waliojiunga na makundi hayo, walisema waliingia huko kwa sababu ya kutaka kuungana na familia zao au marafiki, huku waliosema walijiunga kwasababu za itikadi za kidini, wakishika nafasi ya tatu, ambayo ni sawa na asilimia 17 pekee.

Sababu Kuu

Kiujumla karibu nusu ya waliohojiwa, walitaja sababu tofauti ambazo ziliwasukuma kujiunga, huku asilimia 71 walionesha ni kwa kudhulumiwa, aghalabu na vyombo vya usalama, ikiwa ndio sababu kubwa.

“Ni miongoni mwa ukweli unaouma, kwamba wakati tukijaribu kumaliza makundi yenye itikadi kali, aghalabu mihimili ya dola ndio inakuwa chanzo kingine cha watu kujiunga na makundi haya”. Alisema Steiner

Kinachotokea ndio kinatoa tafsiri sahihi hasa ya kile kinachowasukuma watu kujiunga na mkundi ya kijihadi kwenye nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, na wakati ambao kunashuhudiwa ongezeko kubwa la mashambulio.

Hata hivyo, UNDP inasema kiujumla vifo vilivyotokana na ugaidi duniani imepungua katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, lakini mashambulio katika ukanda wa jangwa la Sahara, yameongezeka mara mbili tangu mwaka 2016.

Kati ya mwaka 2017 na 2021, kulikuwa na mashambulio 4,155 katika mataifa nane yaliyotajwa katika ripoti ya UNDP.

Mwaka 2021, karibu nusu ya vifo vilivyotokana na mashambulio ya kigaidi viliripotiwa kwenye eneo hili, huku zaidi ya theluthi moja vikiripotiwa katika nchi nne, ikiwemo Somalia, Burkina Faso, Niger na Mali.

Kitovu cha itikadi

Steiner anasema eneo la ukanda wa Sahel, limekuwa kitovu cha dunia cha kuibuka kwa makundi yenye misimamo mikali katika miaka ya hivi karibuni.

Mabadiliko haya hayakuifanya Jumuiya ya kimataifa kutazama suala hili kwa umakini, hasa kutokana na ukweli kuwa, macho yote yaligeuka kukabiliana na mlipuko wa uviko19, mabadiliko ya tabianchi na vita ya nchini Ukraine.

UNDP, sasa inataka kuwepo mkakati wa kidunia utakaosaidia kutotoa nafasi kwa makundi haya yenye itikadi kali kupata mwanya au sababu ya kusajili wapiganaji, shirika hili likitaka uwekezaji katika kuboresha maisha ya watoto na vijana ikiwemo kutoa elimu na ushauri nasaha kwa waliojiondoa kwenye makundi hayo.

“Utafiti unaonesha kuwa, wale walioamua kujiondoa kwenye makundi haya, wana uwezekano mdogo sana wa kureje tena au kusajili wenzao”. Amesema Nirina Kiplagat, kiongozi wa jopo kazi la kupambana na itikadi kali duniani.

Ndio maana ni muhimu sana kutoa motisha ili kuwafanya wasirudi tena kwenye makundi hayo, iliongeza kusema ripoti hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.