Pata taarifa kuu

Jenerali Tiani atangaza taasisi mbili za mpito nchini Niger

Jenerali Abdourahamane Tiani, mkuu wa utawala wa kijeshi uliotokana na mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, ameidhinisha siku ya Alhamisi taasisi mbili mpya ya mpito zilizoundwa hivi karibuni, Mahakama ya Nchi na Tume ya Kupambana na Ufisadi.

Ni mara ya kwanza kwa Jenerali Tiani kuonekana hadharani tangu alipompindua Rais Mohamed Bazoum aliyechaguliwa Julai 26. (Picha ya zamani)
Ni mara ya kwanza kwa Jenerali Tiani kuonekana hadharani tangu alipompindua Rais Mohamed Bazoum aliyechaguliwa Julai 26. (Picha ya zamani) © Stringer / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hizo mbili za kuidhinishwa kwa taasisi hizi zilizorushwa moja kwa moja na televisheni ya umma zilifanyika mjini Niamey mbele ya viongozi wa kijeshi, wajumbe wa serikali, viongozi wa kimila, viongozi wa kidini na wanadiplomasia wa kigeni. Wajumbe wa taasisi zote mbili wameapishwa mbele ya Jenerali Tiani, akijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu alipompindua mamlakani Rais Mohamed Bazoum aliyechaguliwa Julai 26.

Mahakama ya Nchi, inayoongozwa na hakimu Abdou Dan Galadima, inachukua nafasi ya Mahakama Kuu na Baraza la Serikali vilivyovunjwa baada ya mapinduzi, kulingana na sheria ambayo hupanga mamlaka ya umma wakati wa kipindi cha mpito kabla ya kufanyika kwa uchaguzi kwa tarehe ambayo bado haijaamuliwa. Kazi  kuu ya Tume ya Kupambana na Ufisadi ni kurejesha mali zote za umma zilizopatikana kwa njia haramu na/au zilizotumiwa vibaya. Inaundwa na mahakimu, maafisa wa jeshi na polisi, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.

Muda wa mpito huo bado haujajulikana, lakini Jenerali Tiani ametangaza muda mfupi baada ya kuchukua madaraka kwamba hautazidi miaka mitatu. Aliahidi kuanzishwa kwa "mazungumzo ya kitaifa" ili kuamua muda wake. Tangu alipopinduliwa, Rais wa zamani Bazoum amezuiliwa katika makaazi yake ya rais. Mnamo Agosti, serikali ya kijeshi ilitangaza nia yake ya kumshtaki kwa "uhaini mkubwa" na "kuhatarisha usalama" wa nchi.

Tangu mapinduzi hayo, Niger imekabiliwa na vikwazo vizito vya kiuchumi na kifedha vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS). Vikwazo hivi husababisha kupanda kwa kasi kwa mfumuko wa bei na uhaba wa baadhi ya bidhaa, ikiwa ni pamoja na madawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.