Pata taarifa kuu

Kiongozi wa Niger Jenerali Abdourahamane Tiani azuru Bamako

Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani, amewasili Alhamisi asubuhi huko Bamako kwa ziara yake ya kwanza ya kimataifa tangu mapinduzi ya Niamey, amebainisha mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Jenerali Tiani anatazamiwa kukaa saa chache mjini Bamako na kukutana na mkuu wa serikali ya Mali, Kanali Assimi Goïta, kwa ziara ya "urafiki na kazi", kulingana na ofisi ya rais wa Mali.
Jenerali Tiani anatazamiwa kukaa saa chache mjini Bamako na kukutana na mkuu wa serikali ya Mali, Kanali Assimi Goïta, kwa ziara ya "urafiki na kazi", kulingana na ofisi ya rais wa Mali. © ORTN
Matangazo ya kibiashara

Mali na Burkina faso, zikiongozwa na wanajeshi walioingia madarakani kupitia mapinduzi mwaka wa 2020 na 2022, walionyesha haraka mshikamano wao na wanajeshi wa Niamey baada ya kutwaa madaraka mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Waliunda pamoja "Muungano wa Mataifa ya Sahel" (AES) ambayo hutoa usaidizi wa pande zote katika tukio la shambulio la uhuru na uadilifu wa eneo la mataifa hayo matatu na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.

Zikiwa zimeungana dhidi ya shinikizo za kimataifa zinazoshinikiza kurejeshwa kwa tawala za kidemokrasia, tawala hizo mbili za kijeshi pia zimeungana dhidi ya wanajihadi ambao mashambulizi yao yanaathiri nchi zao.

Jenerali Tiani anatazamiwa kukaa saa chache mjini Bamako na kukutana na mkuu wa serikali ya Mali, Kanali Assimi Goïta, kwa ziara ya "urafiki na kazi", kulingana na ofisi ya rais wa Mali.

Muda wa kipindi cha mpito nchini Niger bado haujajulikana, lakini Jenerali Tiani alitangaza muda mfupi baada ya kuchukua madaraka kwamba hautazidi miaka mitatu. Nchini Mali, uchaguzi wa urais ambao ulikuwa ufanyike mapema 2024 umeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Alhamisi asubuhi inaonyesha kwamba Bamako itakuwa mwenyeji kuanzia Novemba 23 hadi Desemba 1 wa mikutano miwili ya mawaziri "kwa nia ya kutambua matarajio ya kufanya kazi kwa AES".

Mkutano wa kwanza utawaleta pamoja mawaziri wa uchumi na Biashara mnamo Novemba 25 kwa masuala ya maendeleo ya kiuchumi. Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo tatu watakutana Novemba 30 kwa masuala ya kisiasa na kidiplomasia.

Mikutano hii itatangulia mkutano katika tarehe ya baadaye ya mawaziri wa ulinzi, taarifa hiyo imeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.