Pata taarifa kuu

Niger: Victoria Nuland ajaribu kushawishi viongozi wa mapinduzi bila mafanikio

Victoria Nuland, afisa mkuu wa diplomasia wa Marekani, amekutana mjini Niamey, na viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Niger. Lakini hakuweza kukutana kwa mazungumzo na Abdourahamane Tiani, kiongozi wa waasi, wala Mohamed Bazoum, rais wa Niger ambaye bado anashukiliwa na wanajeshi. Na ziara hii ya kidiplomasia haikuzaa matunda yoyote.

Victoria Nuland, afisa wa diplomasia ya Marekani, alizuru Niamey, Niger, Agosti 7, 2023.
Victoria Nuland, afisa wa diplomasia ya Marekani, alizuru Niamey, Niger, Agosti 7, 2023. AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

"Majadiliano haya yalikuwa ya wazi sana na wakati mwingine yalikuwa magumu": katika mkutano wake na waandishi wa habari kwa simu, Victoria Nuland hakutaka kuficha maudhui ya mazungumzo yake huko Niamey na askari waliochukua mamlaka mnamo Julai 26.

Afisa huyu wa diplomasia ya Marekani amebaini kwamba alikutana na Brigedia Jenerali Moussa Salaou Barmou, mkuu mpya wa jeshi, na maafisa wengine. Lakini hakuweza kuzungumza na kiongozi mkuu wa mapinduzi, Jenerali Abdourahamane Tchiani, au na rais aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum, ambaye bado anashikiliwa na wanajeshi hao.

'Natumai wataweka mlango wazi kwa diplomasia'

Victoria Nuland amesema ametoa "chaguo nyingi" kumaliza mapinduzi, pamoja na ushirikiano mzuri na Marekani "ikiwa kutakuwa na nia nje kwa upande wa maafisa kurejesha utulivu wa kikatiba". "Singesema kuwa jitihada hii imezingatiwa kwa njia yoyote," amekiri, kabla ya kuongeza, "Natumai wataweka mlango wazi kwa diplomasia." Tumetoa pendekezo hili kwao. Tusubiri tuone wataamuaje. "

"Watu waliochukua uamuzi huu (wa mapinduzi) wanaelewa vizuri sana hatari ya uhuru wao inayoletwa na mwaliko kutoka kwa Wagner", ametangaza Victoria Nulan, akimaanisha kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, lililopo hasa katika nchi jirani ya Mali. Kulingana na yeye, viongozi wa mapinduzi wanafahamu "hatari" za muungano na Urusi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.