Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Malema na wabunge wengine 5 wameuziwa kuhudhuria vikao vya bunge

Nairobi – Nchini Afrika Kusini, mwanasiasa wa upinzani Julius Malema na wabunge wengine watano kutoka chama chake Malema cha Economic Freedom Fighters (EFF), wameazuiliwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa kipindi cha mwezi ambapo pia hawatapokea malipo yao wakati wa kipindi hicho.

Wanasiasa hao wa upinzani walipatikana na kosa la kulidharua bunge
Wanasiasa hao wa upinzani walipatikana na kosa la kulidharua bunge Phill Magakoe / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa hao wa upinzani walipatikana na kosa la kulidharua bunge wakituhumiwa kutatiza kikao wakati wa hotuba ya rais Cyril Ramaphosa kwa taifa mwezi Februari.

Malema na wabunge wengine waliondolewa bungeni na walinda usalama baada ya spika kusitisha kikao kilichokuwa kikiendelea wakati huo.

Wanasiasa hao wa upinzani pia wametakiwa kuomba msamaha binafsi kwa bunge na pia kwa rais, spika na raia wa Afrika Kusini kwa kuvuruga hotuba ya mkuu wa nchi, hali ambayo imetajwa kuwa ilitoa taswira mbaya kuhusu taifa hilo.

Marafuku dhidi ya wabunge hao sita itatumika kwa kipindi chote cha mwezi Februari mwaka ujao, hii ikiwa na maana kuwa Malema na wabunge wengine watano watakosa kuhudhuria kikao cha rais Ramaphosa wakati atakapohutubia nchi mwezi huo.

Siku ya Jumatatu wabunge wa EFF wakikataa kuhudhuria vikao vya kamati iliyokuwa inawachunguza baada ya kamati hiyo kukataa ombi lao la kutaka kuhairishwa kwa vikao hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.