Pata taarifa kuu
MAGONJWA HATARI

Hali ya hatari ya Kipindupindu yatangazwa katika mji mkuu wa Zimbabwe

Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, umetangazwa kuwa katika hali ya hatari kutokana na kuzuka tena kwa ugonjwa wa Kipindupindu, ambao tayari umeua watu 51, kuambukiza zaidi ya watu 7,000 nchini humo na unaendelea kuenea, meya mji huo ametangaza siku ya Ijumaa.

Kampeni ya chanjo huko Harare mnamo 2018.
Kampeni ya chanjo huko Harare mnamo 2018. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ian Makone amesema "hali ya sasa  ni ya kutisha", kutokana na idadi ya wagonjwa waliothibitishwa katika wilaya nyingi za mji mkuu, akitambua kuwa sababu kuu ni ukosefu wa maji ya kunywa. "Tumetangaza hali ya hatari kwa sababu hali sasa ni mbaya sana. Ugonjwa huo unaenea katika jiji lote," ameliambia shirika la habari AFP. Kufikia sasa, vifo kumi na viwili vimerekodiwa rasmi mjini Harare.

Zaidi ya visa 7,000 vya watu wanaoshukiwa kuwa wameambukizwa Kipindupindu na karibu vifo 150 vinavyohusishwa na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na 51 vilivyothibitishwa na vipimo vya maabara, hadi sasa vimerekodiwa na mamlaka katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika isiyo na bandari. Viongozi wanasema wako macho, wakihofia kutokea kwa maafa makubwa kama mwaka 2008, wakati kipindupindu kilisababisha maelfu ya vifo.

"Watu wamekuwa wakichimba visima karibu na vyoo vya shimo, hasa katika miji ya watu wenye maisha duni na vitongoji vingine ambavyo havina maji ya bomba. Hii ina maana kwamba maji yao ya kunywa yameambukizwa," Bi. Makone ameliambia shirika la habari la AFP. Manispaa ya  jiji, Wizara ya Afya na mashirika yasio ya kiserikali wameungana kuongeza usambazaji wa maji maradufu katika maeneo yaliyoathiriwa, meya wa mji wa Dakar amesema.

Kulingana na ripoti ya Wizara ya Afya iliyotolewa siku ya Alhamisi jioni, watu 157 kwa sasa wamelazwa hospitalini nchini humo, wakiwemo kumi na sita mjini Harare. Na janga hilo limeenea katika zaidi ya wilaya 17 ambazo kijadi zimeathiriwa na Kipindupindu nchini. Maambukizi ya kuhara kupita kiasi yanayosababishwa na kufyonzwa kwa chakula au maji yaliyochafuliwa na bakteria, Kipindupindu kinazidi kuongezeka barani Afrika, kulingana na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.