Pata taarifa kuu
USAFI-MAZINGIRA

Zimbabwe yachukua hatua madhubuti kudhibiti Kipindupindu kinachoendelea kusambaa

Zimbabwe imetangaza hatua za afya wakati wa mikusanyiko ya watu ili kukabiliana na kuzuka upya kwa ugonjwa wa Kipindupindu. Katika kipndi cha saa 24 zilizopita, wagonjwa wapya 36 wanaoshukiwa kuambulizwa ugonja huo wamerekodiwa na Wizara ya Afya.

Kampeni ya chanjo huko Harare mnamo 2018
Kampeni ya chanjo huko Harare mnamo 2018 © AFP
Matangazo ya kibiashara

Maeneo yote ya nchi yameathiriwa tangu ugonjwa huo ulipozuka tena katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika mapema mwaka huu. Maambukizi ya Kipindipindu yaliyokithiri yanayosababishwa na kufyonzwa kwa chakula au maji yaliyochafuliwa na bakteria, Kipindupindu kinazidi kuongezeka barani Afrika, kulingana na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Nchini Zimbabwe, Wizara ya Afya imerekodi rasmi vifo 30 tangu mwezi wa Februari na zaidi ya wagonjwa 900 walioambukizwa ugonjwa huo. Lakini karibu watu mia moja wanashukiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo na karibu 4,650 wameambukizwa.

Maeneo ya mijini nchini humo, ambayo yamekuwa katika mzozo mkubwa wa kiuchumi kwa takriban miaka ishirini, ambapo miundombinu ya afya na mifumo ya usambazaji wa maji ya kunywa mara nyingi hutelekezwa, huathiriwa mara kwa mara na Kipindupindu.

Halmashauri ya manispaa ya Harare imeshauri, katika notisi iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, dhidi ya kupeana mikono, kula kwenye mikusanyiko ya watu na kununua chakula kutoka kwa wachuuzi wasio rasmi. Takriban kilomita 340 kutoka mji mkuu, katika wilaya ya Zaka, viongozi wa eneo hilo wamepiga marufuku mikusanyiko ya watu ambayo sasa iko chini ya idhini kutoka kwa Wizara ya Afya.

Mwaka 2008, kipindupindu kiliua watu wasiopungua 4,000 nchini Zimbabwe na kuambukiza watu 100,000. Pamoja na kudorora kwa uchumi, hospitali nyingi za umma zinakumbwa na uhaba wa dawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.