Pata taarifa kuu

Sudan: Daraja la kimkakati la Shambat linalounganisha Khartoum na vitongoji vyake laharibiwa

Pande mbili zinazokinzana nchini Sudani zinashumiana kila upande ukishtumu mwingine kwa kuhusika na uharibifu wa daraja la Shambat linalounganisha Khartoum-Kaskazini na Omdurman, katika vitongoji vya magharibi. 

Moshi unafuka Omdurman, karibu na Daraja la Halfaya, wakati wa mapigano kati ya vikosi vy wanamgambo wa RSF na jeshi kama inavyoonekana kutoka Khartoum Kaskazini, Sudan Aprili 15, 2023.
Moshi unafuka Omdurman, karibu na Daraja la Halfaya, wakati wa mapigano kati ya vikosi vy wanamgambo wa RSF na jeshi kama inavyoonekana kutoka Khartoum Kaskazini, Sudan Aprili 15, 2023. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, jeshi la Sudan, likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, limewashutumu "wanamgambo wa waasi" wa RSF kwa "kuharibu daraja la Shambat mapema leo [Jumamosi] asubuhi". Kwa upande wao, Vikosi vya Msaada wa Haraka (FSR) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo pia vimekanusha shutuma hizi katika taarifa kwa vyombo vya habari na kulituhumu jeshi la mpinzane wake kuwa ndilo limehusika.

Ghasia nchini Sudan zakithiri, Umoja wa Mataifa waonya

Baada ya miezi saba ya vita na kuongezeka kwa mapigano hivi karibuni kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF, ghasia nchini Sudan zimekithiri na kuwa "uovu mtupu", afisa wa Umoja wa Mataifa alionya siku ya Ijumaa, akihofia hasa kuhusu mashambulizi ya kikabila huko Darfur.

Uporaji

Kulingana na UNHCR, katika siku za hivi karibuni, "zaidi ya watu 800 wameuawa na makundi yenye silaha huko Ardamata, Darfur Magharibi, eneo ambalo hadi sasa haliathiriwi sana na vita." Ardamata pia ilikuwa inawapa hifadhi watu waliolazimika kutoroka makazi yao, ambapo karibu makazi 100 yaliharibiwa, kulingana na UNHCR. Hata hivyo, visa vingi vya uporaji - hasa wa vitu vya msaada vya shirika - vimeripotiwa katika eneo hilo.

UNHCR imesema inasikitishwa sana na ripoti za unyanyasaji wa kingono, utesaji, mauaji ya kiholela, unyang'anyi wa raia na kulenga watu wa makabila, pamoja na ripoti kwamba maelfu ya watu waliokimbia makazi yao walilazimika kukimbia kambi ya El-Geneina.

Shirika hilo linajiandaa kwa wimbi jipya la wakimbizi nchini Chad. limesema, "wale ambao wamefanikiwa kukimbia na kufaulu kuvuka mpaka wanawasili kwa wingi", akibainisha kuwa "zaidi ya watu 8,000 wamekimbilia nchi jirani ya Chad katika wiki iliyopita pekee - idadi ambayo huenda huenda iko juu kutokana na ugumu wa kujiandikisha kwa "wakimbizi wapya". 

Vita kati ya mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, na vikosi vya Msaada wa Haraka (FSR) vya Jenerali Mohamed Hamdane Dagloa ambavyo vilianza Aprili 15, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000, kulingana na makadirio ya shirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data Project (ACLED). Vita hivyo pia vimeharibu miundombinu mingi na kuwafanya zaidi ya watu milioni 4.8 kuwa wakimbizi ndani ya Sudan na milioni 1.2 katika nchi jirani, kulingana na UNHCR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.