Pata taarifa kuu

Vita nchini Sudan: Mapigano yanaendelea Khartoum na Darfur

Miili ya watu waliovalia sare za kijeshi imetapakaa katika mitaa ya Omdurman, nje kidogo ya mji mkuu wa Sudan, mashahidi wameripoti siku ya Alhamisi, wakati Umoja wa Mataifa ukielezea wasiwasi juu ya kuongezeka kwa mapigano katika eneo la Darfur katika mwezi wa saba wa vita kati ya jeshi na vikosi vya wanamgambo wa RSF.

Vita kati ya jeshi na FSR ya Jenerali Daglo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000 na kuwahamisha zaidi ya watu milioni 6, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Vita kati ya jeshi na FSR ya Jenerali Daglo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000 na kuwahamisha zaidi ya watu milioni 6, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yanaendelea mjini Khartoum na vitongoji vyake pamoja na Darfur, magharibi mwa nchi hiyo, huku duru mpya ya mazungumzo yaliyofadhiliwa na Saudi Arabia na Marekani ikimalizika wiki hii bila mafanikio.

"Miili ya watu waliovalia sare za kijeshi imetanda katika mitaa ya katikati mwa jiji baada ya mapigano ya jana (Jumatano)," walioshuhudia huko Oumdurman wameliambia shirika la habari la AFP, wakihojiwa kwa simu kutoka Wad Madani, kusini mwa Khartoum. Wengine wameripoti kwamba bomu lilianguka kwenye hospitali ya AlNau kaskazini mwa Omdurman, kituo cha mwisho cha matibabu katika mkoa huo, na kumuua "muhudumu" wa afya. Umoja wa Mataifa pia umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kibinadamu huko Darfur.

"Mamia ya maelfu ya raia na watu waliokimbia makazi yao sasa wako katika hatari kubwa huko El-Facher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, wanakabiliwa na kuzorota kwa kasi kwa hali ya usalama (na) ukosefu wa chakula na maji," ameandika kwenye X (zamani ikiitwa Twitter. ) Toby Harward, naibu mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa huko Darfur. "Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na jeshi la Sudan vinapigania kudhibiti mji huo, na hii itakuwa na athari mbaya kwa raia," ameongeza.

Shuhuda za mauaji katika jimbo la Darfur Magharibi

Ubalozi wa Marekani, kwa upande wake, umeelezea "wasiwasi wake mkubwa katika shuhuda zinazoripoti ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na RSF" huko Darfur. Unaripoti "hasa ​​mauaji katika eneo la Ardmata, katika jimbo la Darfur Magharibi" na una wasiwasi kuhusu ukweli kwamba viongozi na wanachama wa Massalit, mojawapo ya makabila madogo zaidi yasiyo ya Kiarabu huko Darfur Magharibi, "wanalengwa".

Baraza la Uhuru, mamlaka ya juu zaidi nchini, lilitangaza siku ya Jumatatu kifo cha "nguzo ya utawala wa kiraia huko Darfur Magharibi (...), aliyeuawa" na wanamgambo wa RSF ambao "walishambulia nyumba kadhaa katika eneo la Ardmata. "Mtoto wake wa kiume na wajukuu zake wanane pia waliuawa," inaongeza taasisi hii inayoongozwa na mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane.

Vita kati ya jeshi na FSR ya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo ambayo ilianza Aprili 15 vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000 kulingana na makadirio ya Shirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data Project (Acled). Vita pia limesababisha zaidi ya watu milioni 6 kuyahama makaazi yao na kuharibu miundombinu mingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.