Pata taarifa kuu

Sudan: Zaidi ya raia 20 wauawa kwa kuangukiwa na makombora kwenye soko Omdurman

Zaidi ya raia 20 waliuawa Jumapili jioni, Novemba 5, wakati makombora yalipoanguka kwenye soko huko Omdurman, kitongoji kilicho karibu na Khartoum, mji mkuu wa Sudan, shirika moja lisilo la kiserikali limetangaza.

Khartoum, Sudan, Aprili 15, 2023, karibu na daraja la Halfaya juu ya Mto Nile linalotenganisha Khartoum na Omdurman: moshi angani unashuhudia mapigano kati ya wanamgambo wa RSF na jeshi la kawaida.
Khartoum, Sudan, Aprili 15, 2023, karibu na daraja la Halfaya juu ya Mto Nile linalotenganisha Khartoum na Omdurman: moshi angani unashuhudia mapigano kati ya wanamgambo wa RSF na jeshi la kawaida. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa kutoka kwa Kamati ya Wanasheria wanaounga mkono Demokrasia ambayo inaandika kumbukumbu za vifo vya kiraia na ukiukwaji wa haki za binadamu katika mzozo huo, "wakati wa majibizano makali ya risasi kati ya wapiganaji, makombora yalianguka kwenye soko la Omdurman." "Zaidi ya raia 20 waliuawa na wengine kujeruhiwa," inasema taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Siku moja kabla, angalau raia 15 waliuawa na "baada ya kuangukiwa na makombora kwenye nyumba zao" huko Khartoum, chanzo cha hospitali kimesema.

Vita kati ya jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohamed Hamdane Daglo Aprili 15 vilivyoanza Aprili 15, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 9,000, kulingana na makadirio ya shirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data Project (Acled), huku wadadisi wakisema idadi hiyo inaweza kuwa juu zaidi.

Kambi zote mbili zimeshindwa kuafikiana kusitisha mapigano au kuafikiana kuketi kwenye meza ya mazungumzo. Mazungumzo kati ya wapiganaji hao yalifanyika katika mji wa Jeddah wa Saudia. Yalilenga "kurahisisha utoaji wa misaada ya kibinadamu, kuanzisha usitishaji mapigano na hatua nyingine za kujenga imani, na kuelekea katika usitishaji wa kudumu wa uhasama," kulingana na Riyadh.

Majaribio ya awali ya upatanishi yalisababisha mapatano mafupi tu, ambayo yote yalikiukwa kimfumo. Majenerali al-Burhan na Daglo walichagua badala ya vita vya ugomvi, wakitumai kupata maafikiano makubwa katika meza ya mazungumzo, wamesema wataalam.

Mzozo huo pia umewakosesha makazi zaidi ya watu milioni 6. milioni 1.2 kati yao wamekimbilia katika nchi jirani. Kulingana na Umoja wa Mataifa, wanawake na wasichana wanatekwa nyara na kuwa watumwa kila siku huko Darfur. Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi anatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufadhili mahitaji ya kibinadamu yanayoongezeka.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.