Pata taarifa kuu

Sudan: Niko tayari kwa mazungumzo ya kumaliza mapigano: Mkuu wa jeshi

Nairobi – Mkuu wa jeshi la Sudan ameliambia shirika la utangazaji la Uingereza kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na kamanda wa kikosi cha RSF kinachopigana na maofisa wake nchini humo.

Akizungumza na BBC kando na mkutano ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Jenerali amekana madai ya kuwa vikosi vyake vilikuwa vinawalenga raia katika mapigano hayo
Akizungumza na BBC kando na mkutano ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Jenerali amekana madai ya kuwa vikosi vyake vilikuwa vinawalenga raia katika mapigano hayo REUTERS - EDUARDO MUNOZ
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema yuko tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo na mpizani wake wa kijeshi Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, mkuu wa RSF.

Makundi hayo ya kijeshi yamekuwa yakipigana tangu mwezi April, makabiliano ambayo Umoja wa Mataifa umesema yamesababisha mauji ya watu zaidi ya elfu tano.

Watu zaidi ya milioni tano tayari wameripotiwa kuyakimbia makazi yao kutokana na vita hivyo, wengi wao wakiishi katika kambi za wakimbizi.

Jenerali Al Burhan(kulia) amekuwa akipambana na mkuu wa wapiganaji wa RSF Hamdan Dagalo(kushoto)
Jenerali Al Burhan(kulia) amekuwa akipambana na mkuu wa wapiganaji wa RSF Hamdan Dagalo(kushoto) © AP

Akizungumza na BBC kando na mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Jenerali amekana madai ya kuwa vikosi vyake vilikuwa vinawalenga raia katika mapigano hayo.

Kiongozi huyo amesema yuko na uhakika na kupata ushindi katika vita hivyo, akieeleza kwamba amelazimika kuhamisha makao makuu yake kutoka jijini Khartoum hadi hadi Port Sudan kutokana na mapigano yanayoendelea.

Burhan amesisitiza kuwa atafanya mazungumzo na Dagalo – maarufu kama Hemedti iwapo atakubali kuwalinda raia kwa mujibu wa makubaliano yalioafikiwa katika mazungumzo ya pande zote mjini Jeddah, Saudi Arabia, mwezi Mei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.