Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Zimbabwe: Mbunge wa upinzani atekwa nyara, ateswa, kabla ya kupatikana akiwa uchi

Mbunge wa upinzani nchini Zimbabwe ametekwa nyara Jumatano asubuhi, akateswa kisha kutelekezwa akiwa uchi kando ya barabara, chama chake kimebaini, katika muktadha wa mvutano unaodumu tangu uchaguzi wenye utata katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika mwezi Agosti.

Mamlaka iliongeza vikosi vya usalama kabla ya uchaguzi. Hapa, maafisa wa polisi wakizingira lililobeba wapinzani, kabla ya kufikishwa mahakamani, wakishutumiwa kwa kuzorotesha shughuli mbalimbali, mjini Harare, Agosti 17, 2023.
Mamlaka iliongeza vikosi vya usalama kabla ya uchaguzi. Hapa, maafisa wa polisi wakizingira lililobeba wapinzani, kabla ya kufikishwa mahakamani, wakishutumiwa kwa kuzorotesha shughuli mbalimbali, mjini Harare, Agosti 17, 2023. © Tsvangirayi Mukwazhi / AP
Matangazo ya kibiashara

Takudzwa Ngadziore, 25, alitekwa nyara na watu wenye silaha karibu na nyumba yake katika mji mkuu Harare alipokuwa akielekea Bungeni, kulingana na Muungano wa Mabadiliko ya Wananchi (CCC).

Bw Ngadziore, mbunge mwenye umri mdogo zaidi nchini Zimbabwe, aliweza kutangaza moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii nyakati zilizosababisha madai ya kutekwa nyara kwake. Katika kipande kifupi cha video, mwanasiasa huyo aliyekuwa na mfadhaiko, akiwa amevaa tai, anaonekana akitazama kamera huku akisema "Nafuatwa" kwa lugha ya kienyeji ya Kishona, kabla ya kumuonyesha mtu aliyejihami na bunduki aina ya Kalashnikov na aliyevaa kofia nyeusi akimfuata.

Alipatikana saa kadhaa baadaye, mwili wake ukiwa umefunikwa na mikato, takriban kilomita arobaini karibu na kijiji cha Mazowe, rafiki yake aliyekwenda kumchukua ameliambia shirika la habari la AFP.

CCC, chama kikuu zaidi cha upinzani, kimenyooshea kidole cha lawama chama tawala cha ZANU-PF, kikisema utekaji nyara huo ni sehemu ya kampeni pana ya vitisho dhidi ya wafuasi wake. Polisi na ZANU-PF hawakujibu mara moja ùadaia ya chma hiki cha upinzani.

"Kuendelea kulengwa kwa wanachama mashuhuri (wa CCC) kunalenga kuzua hofu miongoni mwa watu kwa ujumla," msemaji wa chama Promise Mkwananzi amesea kwenye ukurasa wake wa X. "Huu ni mfano mwingine wa "machafuko ya kiholela ambayo yameikumba Zimbabwe tangu kufanyka kwa uchaguzi uliovurugwa."

Bw. Ngadziore alikuwa amelazwa hospitalini, pengine akisumbuliwa na mkono na goti lililovunjika, amesema rafiki yake ambaye alipendelea kutotajwa jina.

Vyombo vya habari vya ndani na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesisitiza kwamba waliomteka huenda ni vikosi vya usalama vya Zimbabwe. Hili ni tukio la pili la hivi karibuni la aina hii: wiki iliyopita, James Chidhakwa, mbunge wa zamani wa CCC, alitekwa nyara na kuteswa kabla ya kupatikana saa chache baadaye katika viunga vya mji mkuu wa Harare, akiwa amenyolewa nywele.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.