Pata taarifa kuu

Baada ya mapinduzi, uchumi wa Niger wadidimia

Miezi mitatu baada ya mapinduzi yaliyompindua Rais Bazoum nchini Niger, vikwazo vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi na kusimamishwa kwa ufadhili wa kimataifa vinadhoofisha matarajio ya kiuchumi ya nchi miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani.

Kiasi cha msaada wa bajeti inayotolewa kwa Niger sasa inakadiriwa kuwa dola milioni 254, ikilinganishwa na dola bilioni 1.166 zilizopangwa kabla ya mapinduzi.
Kiasi cha msaada wa bajeti inayotolewa kwa Niger sasa inakadiriwa kuwa dola milioni 254, ikilinganishwa na dola bilioni 1.166 zilizopangwa kabla ya mapinduzi. © AP
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya (EU), mshirika mkuu wa Niger, ulikuwa umetenga euro milioni 503 (dola milioni 554) "kuboresha utawala, elimu na ukuaji endelevu nchini Niger kwa kipindi cha mwaka 2021 na 2024", kulingana na tovuti yake. Lakini kama washirika wengine kama vile Ufaransa, Umoja wa Ulaya ulitangaza "kusitishwa mara moja" msaada wake wa kibajeti kufuatia mapinduzi hayo.

Kwa ujumla, kiasi cha msaada wa bajeti iliyotolewa kwa Niger sasa inakadiriwa kuwa dola milioni 254 kutolewa, ikilinganishwa na dola bilioni 1.166 zilizopangwa kabla ya mapinduzi, kulingana na utafiti wa Benki ya Dunia (WB) na shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP).

Kwa upande wa ufadhili wa miradi ya maendeleo, "dola milioni 82 tu (0.55% ya Pato la Taifa) zililipwa mwaka 2023, ikilinganishwa na fedha zinazotarajiwa sawa na dola milioni 625  (3.6% ya Pato la Taifa)", kulingana na utafiti ambao unaonyesha kuwa kusitishwa huku "kutakuwa na uzito kwa kiasi kikubwa kwa uwezo wa nchi wa kutekeleza miradi na kutekeleza bajeti".

Takwimu hizi zilizoanzishwa mwanzoni mwa mwezi Oktoba hazizingatii kusimamishwa na Washington kwa programu zake nyingi za msaada kwa nchi, kwa kiasi cha karibu dola milioni 500.

Bajeti iliyopunguzwa

Ni asilimia 62 pekee ya bajeti ya Niger inafadhiliwa na mapato yake ya ndani, kulingana na Umoja wa Ulaya. Utawala wa kijeshi ulitangaza mapema mwezi Oktoba kupunguza 40% katika bajeti ya kitaifa ya 2023, kutokana na "vikwazo vizito vilivyowekwa na mashirika ya kimataifa na ya kikanda", ambayo "yanaiweka nchi  kwa kupoteza kiasi kikubwa kwa mapato ya nje na ya ndani" .

Vikwazo vya ECOWAS vinaizuia Niger kufikia soko la kifedha la kikanda la Umoja wa Kiuchumi na Fedha wa Afrika Magharibi (WAEMU) ili kufadhili bajeti yake na kufanya miamala ya kibenki. Kwa kujibu, mamlaka ya Niger iliwataka walipa kodi kulipa kodi kwa pesa taslimu, badala ya kuziweka kwenye akaunti ya Hazina, iliyozuiliwa na vikwazo.

kutokana na kushuka kwa mapato kwa kiasi kikubwa, serikali inatanguliza malipo ya mishahara ya watumishi wa umma, kwa kuathiri uwekezaji wa umma, kulingana na Benki ya Dunia, WB. Benki ya Dunia inaongeza kuwa "utawala mpya umekosa malipo kadhaa ya riba (kwenye deni lake, maelezo ya Mhariri), hali hii tayari imesababisha malimbikizo na huenda ikasababisha kusitishwa" kwa usaidizi mwingine wa kifedha wa kimataifa.

Miundombinu chini ya tishio

Nigeria ilitangaza kusimamisha usambazaji wake wa umeme kwa Niger, ambayo iliwakilisha 71% ya matumizi ya nchi hiyo kabla ya mapinduzi. Shirka la umeme ya Nigerien (Nigelec) linasimamia tu kukidhi kati ya 25% na 50% ya mahitaji kulingana na ukanda, na hali yake ya kifedha inazidi kuzorota, kulingana na WB.

Miradi kadhaa ya miundombinu pia inatishiwa na kusimamishwa kwa ushirikiano wa Magharibi. Uanzishaji wa mtambo wa nishati ya jua wa Gorou Banda, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), umecheleweshwa.

Kazi katika bwawa la Kandadji, linalofadhiliwa na AFD, Benki ya Maendeleo ya Afrika Magharibi (BOAD) na Benki ya Uwekezaji ya ECOWAS (EBID), pia imesimama. "Ucheleweshaji wa miradi ya miundombinu ya umeme utazuia kuongezeka kwa upatikanaji wa umeme wa bei nafuu na wa uhakika kwa kaya na viwanda," inahakikishia WB, katika nchi ambayo ni asilimia 20 tu ya watu wanapata umeme.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.