Pata taarifa kuu

Misri: Watu 35 wameangamia katika ajali iliyotokea kati ya basi na magari kadhaa

Takriban watu 35 wamefariki na wengine 53 kujeruhiwa leo Jumamosi katika baada ya magari gogongana kwenye barabara inayounganisha Cairo na Alexandria katika pwani ya kaskazini mwa Misri, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Picha zilizochapishwa mtandaoni kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha lori lililopinduliwa kwenye barabara ya mwendokasi, ambayo lami imechomwa kwa kiasi. Mbali zaidi, angalau basi moja na basi dogo huonekana kwa kiasi kikubwa zimeteketea kwa moto, kama vile magari mengi, mengine yakiwa bado yanawaka.
Picha zilizochapishwa mtandaoni kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha lori lililopinduliwa kwenye barabara ya mwendokasi, ambayo lami imechomwa kwa kiasi. Mbali zaidi, angalau basi moja na basi dogo huonekana kwa kiasi kikubwa zimeteketea kwa moto, kama vile magari mengi, mengine yakiwa bado yanawaka. REUTERS/Asmaa Waguih
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imegharimu "maisha ya watu 35, angalau 18 kati yao waliteketea kwa moto," limesema Gazeti la kila siku la Al-Ahram, ambalo limechapisha orodha ya "angalau watu 53 waliojeruhiwa."

Ajali za za barabarani hutokea mara kwa mara nchini Misri ambapo barabara mara nyingi hazitunzwi vizuri na sheria za barabarani na desturi ya uendeshaji mzuri haziheshimishwi.

Picha zilizochapishwa mtandaoni kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha lori lililopinduliwa kwenye barabara ya mwendokasi, ambayo lami imechomwa kwa kiasi. Mbali zaidi, angalau basi moja na basi dogo huonekana kwa kiasi kikubwa zimeteketea kwa moto, kama vile magari mengi, mengine yakiwa bado yanawaka.

Pande zote, watazamaji na mistari ya magari wanangoja, huku kukiwa na mayowe na umati wa watu katika wingu zito la moshi mweusi.

Watu 7,000 walifariki katika ajali za barabarani mnamo mwaka 2021 katika nchi hii yenye watu wengi zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu, ambayo ina wakaazi milioni 105.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.