Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Liberia: Matokeo ya mwisho yathibitisha duru ya pili kati ya George Weah na Joseph Boakai

George Weah na Joseph Boakai watachuana katika duru ya pili iliyo karibu sana, kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi siku ya Jumanne.

Mlinzi akiangalia masanduku ya kura wakati wa uchaguzi wa urais huko Monrovia, Liberia, Oktoba 10, 2023.
Mlinzi akiangalia masanduku ya kura wakati wa uchaguzi wa urais huko Monrovia, Liberia, Oktoba 10, 2023. REUTERS - CARIELLE DOE
Matangazo ya kibiashara

Takriban kura 7,000 zinawatenganisha wawili hao. George Weah alipata 43.83% ya kura na Joseph Boakai, 43.44% wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Liberia. Matokeo haya yanathibitisha mwelekeo uliotolewa na matokeo ya muda katika wiki iliyopita. Ni matokeo tu kutoka kwa vituo vichache vya kupigia kura katika kaunti za Nimba, Sinoe, na Montserrado yaliyokuwa yanasubiriwa, kwani wapiga kura katika maeneo hayo walilazimika kupiga kura tena.

Hakuna hata mmoja kati ya wagombea wawili wakuu aliyeweza kukusanya idadi ya kura zinazohitajika ili kupata wingi kamili. Kinyang'anyiro hicho sasa kiko wazi kurejesha kura za wagombea walioondolewa katika duru ya kwanza. Kati ya wagombea urais 18wanaosalia, hakuna anayezidisha 3% ya kura. Mgombea wa nafasi ya tatu, Edward Appleton, yuko nyuma sana kwa wapinzani wote wawili. Alipata 2.2% ya kura. Zimesalia wiki tatu kabla ya duru ya pili inayotarajiwa kufanyika Novemba 14. Wakati huu, kila mmoja wa wagombea atalazimika kuwashawishi wapiga kura wa wagombea wadogo.

George Weah, licha ya umaarufu wake mkubwa miongoni mwa vijana, amewaacha wengi wakiwa wamekata tamaa. Hali ya maisha ya watu masikini zaidi haijaboreka na ufisadi umeongezeka chini ya uongozi wake. Joseph Boakai aliahidi kuboresha maisha ya watu maskini zaidi, lakini ameanzisha ushirikiano na watawala wa ndani, hasa mbabe wa zamani wa vita Prince Johnson, hali ambayo inaweza kumnufaisha na kupelekea kura kura alizopata katika duru ya kwanza zinaongezeka.

Kulingana na tume ya uchaguzi, karibu kura 114,000 zilibatilishwa wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi. Hasara inayohusishwa na ukosefu wa uwazi wa uchaguzi huu, anabaini mtaalamu wa masala ya siasa Abdullah Kiatamba. "Mchakato unapaswa kuwa rahisi zaidi na angavu zaidi katika raundi ya pili," anasema mtafiti huyu. Na kiwango cha ushiriki kilikuwa 58.86%. Hapa pia, itabidi kutafuta kura za wale ambao hawakujitokeza katika duru ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.