Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

George Weah amshinda mshindani wake katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Liberia

Rais anayemaliza muda wake George Weah anaongoza kwa kura  ndo katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Liberia kwa 43.83% ya kura, dhidi ya mshindaniwake Joseph Boakai aliyepata 43.44%, kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotolewa Jumanne na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.

George Weah bado anapendwa na baadhi ya vijana, lakini pia amewakatisha tamaa wengi katika muhula wake wa kwanza.
George Weah bado anapendwa na baadhi ya vijana, lakini pia amewakatisha tamaa wengi katika muhula wake wa kwanza. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 10 yanaonyesha kuwa hakuna orodha ya wagombea urais iliyopata kura 50 + 1," ametangaza Bi Davidetta Browne-Lansanah, huku akitangaza kwamba duru ya pili itafanyika mnamo Novemba 14. Pambano hili kati ya wagombea hao wawili ni kisasi cha uchaguzi wa 2017 alioshinda Bw. Weah, nyota wa zamani wa soka. Hakuna hata mmoja wa wagombea wengine 18 aliyepata 3% ya kura.

Tume ya uchaguzi imesema ushiriki ulikuwa wa "kihistoria" na baada ya wapiga kura wa 78.86% uchaguzi wa Oktoba 10, uchaguzi ambao ulifanyika vurugu yoyote na kupongezwa na waangalizi wa kimataifa.

Bw. Weah bado anapendwa na baadhi ya vijana, lakini pia amewakatisha tamaa wengi katika muhula wake wa kwanza. Wengi wanamshutumu kwa kutotimiza ahadi zake. Hali ya maisha ya watu masikini zaidi haijaboreka na ufisadi umeongezeka.

Bw. Boakai, aliyekuwa makamu wa rais kuanzia 2006 hadi 2018, amekuwa mpinzani mkuu katika siasa za kitaifa kwa takriban miongo minne. Ameahidi kurejesha sura ya nchi, kuendeleza miundombinu na kuboresha maisha ya watu wengi wawanaokabiliwa na umasikini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.