Liberia: Zoezi la kuhesabu kura limeanza
Nairobi – Shughuli ya kuhesabu kura inaendelea nchini Liberia baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji kura, kumchagua rais mpya na wabunge siku ya Jumanne.
Imechapishwa:
Raia katika taifa hilo la Afrika Magharibi walipiga kura kumchagua rais, wajumbe wa baraza la wawakilishi na baadhi ya wabunge wa Seneti.Rais aliye madarakani na mwanasoka wa zamani George Weah, ambaye anawania muhula wa pili, ndiye anayepigiwa upatu kuibuka mshindi.
Weah, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea wengine 19.
Makamu wa rais wa zamani Joseph Boakai na mfanyibiashara Alexander Cummings, ametajwa kuwa mpinzani mkuu wa rais Weah.
Hali ya wasiwasi ilishuhudiwa wakati wa kipindi cha kampeni, vurugu zikishuhudiwa katika jimbo la Lofa kati wa wafuasi wa rais anayeondoka madarakani na wafuasi wa upinzani.
Weah aliingia mdarakani mwaka wa 2017 baada ya majaribio mawili ya hapo awali kutofanikiwa.
Tume ya uchaguzi inatarajiwa kuanza kuchapisha matokeo ya kwanza leo.