Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Raia wa Liberia wanapiga kura kumchagua rais wao mtarajiwa

Raia wa Liberia wanapiga kura tangu asubuhi ya Jumanne kumchagua rais wao mtarajiwa, huku George Weah anayemaliza muda wake, nyota wa zamani wa kandanda duniani, anapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo akipambana na washindani 19.

Uchaguzi huu ni wa kwanza kufanyika bila kuwepo kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, ulioundwa mwaka 2003 ili kuhakikisha amani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya 250,000 kati ya mwaka 1989 na 2003.
Uchaguzi huu ni wa kwanza kufanyika bila kuwepo kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, ulioundwa mwaka 2003 ili kuhakikisha amani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya 250,000 kati ya mwaka 1989 na 2003. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wapiga kura milioni 2.4 wameitwa kupiga kura katika nchi hii ndogo inayozungumza Kiingereza katika Afrika Magharibi ambayo ina ndoto ya maendeleo na amani baada ya miaka mingi yenye vita na magonjwa ya milipuko. Mbali na rais wao, pia watachaguwa wawakilishi wao na maseneta 15.

Mamia ya watu walijaa chini ya jua mbele ya vituo vya kupigia kura mjini Monrovia, vilivyowekwa shuleni, kuanzia saa 7:00 asubuhi (saa za Afrika Magharibi), saa moja kabla ya ufunguzi, wamebaini waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP.

"Napiga kura kwa manufaa ya nchi yangu. Natarajia amani na maendeleo. Nadhani utakuwa uchaguzi wa karibu kati ya Weah na Boakai", mpinzani wake mkuu amesema mbele ya moja ya ofisi hizo Agostina Momo, mwenye umri wa miaka 18, ambaye anapiga kura kwa mara ya kwanza.

"Ni wajibu wangu wa kikatiba kupiga kura, kwa ajili ya mustakabali wa watoto wangu, wajukuu zangu. Natumai kuwa rais ajaye atakuwa mwadilifu zaidi kwa nchi yetu," amesema Augustus Okai, 54, wa kwanza kupiga kura katika kituo chake cha kupigia kura ili kumchagua rais, mbunge wake na seneta wake.

Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa hadi saa 6:00 jioni. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itaanza kutoa matokeo hadharani kuanzia siku ya Jumatano wakati zoezi la uhesabuji kura kura likiendelea na itatangaza matokeo ya mwisho ndani ya siku 15.

Uchaguzi huu ni wa kwanza kufanyika bila ya kuwepo kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, ulioundwa mwaka 2003 ili kuhakikisha amani baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 250,000 kati ya mwaka 1989 na 2003.

Makabiliano kati ya chama tawala na wapinzani wakati wa kampeni yalisababisha vifo vya watu watatu kaskazini magharibi. Makabiliano mapya yalisababisha angalau watu kadhaa kujeruhiwa wakati wa gwaride la mwisho la kampeni ya Bw. Weah siku ya Jumapili mjini Monrovia, na kuibua hofu ya ghasia za baada ya uchaguzi.

Waangalizi

Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi na Marekani zimetuma waangalizi katika eneo ambalo demokrasia inatiliwa shaka na kuzidishwa kwa mapinduzi ya kijeshi.

Bw. Weah, aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2017, ana umaarufu mkubwa kati ya vijana.

Siku ya Jumapili, alikusanya umati mkubwa huko Monrovia, ikilinganishwa na mikutano ya washindani wake wengine. "Tunamtaka kwa miaka sita zaidi. Alitunza amani, alijenga barabara, alilipa karo ya shule. Yeye ni kiongozi mzuri," amesema Theresa Sneh, 48.

Mshambulizi huyo nyota wa zamani ndiye mgombea aliyeonekana zaidi wakati wa kampeni. Picha yake huko Monrovia iko kila mahali, ikiwa na kauli mbiu "Ushindi kwa duru moja".

Katika hotuba yake, alitetea rekodi yake ya kiuchumi, ujenzi wa shule, hospitali, upatikanaji wa umeme kwa idadi kubwa zaidi. Aliahidi kujenga barabara mpya, kuunda nafasi za kazi na kuendeleza "vita" dhidi ya rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.