Pata taarifa kuu

Marekani kutangaza vikwazo kwa watakaohujumu uchaguzi wa Liberia

Marekani imeonya kuwa itatangaza vikwazo vya usafiri kwa yeyote yule atakayehujumu zoezi la uchaguzi mkuu wa mwezi ujao nchini Liberia.

Rais wa sasa George Weah anawania uchaguzi huo kutafuta nafasi ya kuiongoza Liberia kwa muhula wa pili
Rais wa sasa George Weah anawania uchaguzi huo kutafuta nafasi ya kuiongoza Liberia kwa muhula wa pili AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Washington imesema hatua hiyo inawalenga watu wanaohujumu demokrasia kwenye taifa hilo la Afrika kupitia udaganyifu, watu watakaojihusisha na machafuko ama kujihusisha na mambo mengine yanayoweza kuhitilafiana na matokeo ya uchaguzi huo.

Aidha Washington imesema kuwa hatua hiyo pia inalenga kuonyesha uungwaji mkono wake kwa raia wa Liberia walio na matarajio ya kushiriki uchaguzi wa huru na haki.

Licha ya onyo hilo, Marekani haikuweka wazi majina ya watu wanaolengwa kwa mpango huo.

Rais wa sasa George Weah anawania uchaguzi huo kutafuta nafasi ya kuiongoza Liberia kwa muhula wa pili.

Weah, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa kiongozi wa upinzani Joseph Boakai aliyeshindwa katika uchaguzi mkuu wa uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.