Pata taarifa kuu

Sudan: Wapiganaji wa RSF waendeleza mashambulio kwenye makao makuu ya jeshi

Nairobi – Nchini Sudan, kwa siku ya pili, wanamgambo wa RSF wameendeleza mashambulio kwenye makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.

Vita hivyo vilivyoanza Arprili 15, vimeendelea wakati kiongozi wa kijeshi Fattah al-Burhan akiendelea na ziara yake katika nchi za nje
Vita hivyo vilivyoanza Arprili 15, vimeendelea wakati kiongozi wa kijeshi Fattah al-Burhan akiendelea na ziara yake katika nchi za nje © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mapigano makali sasa yanaendelea, katika maeneo yanayozingira makao makuu ya jeshi kwa mujibu wa wakaazi wa Khartoum, wanaosema wanasikia milio ya risasi na moto mkubwa yakiteketezwa majengo karibu na êneo hilo.

Jengo refu, kunakopatikana ofisi za shirika la petroli na wizara ya haki, ni baadhi ya majengo yaliyoharibiwa kutokana na mapigano hayo yaliyoanza Jumamozi iliyopita.

Vita hivyo vilivyoanza Arprili 15, vimeendelea wakati kiongozi wa kijeshi Fattah al-Burhan akiendelea na ziara yake katika nchi za nje, wakati huu akikutana na rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Watu zaidi ya 7,500 wameuawa katika vita hivyo kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa, huku wengine zaidi ya Milioni 5 wakiyakimbia makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.