Pata taarifa kuu

Mali: Waasi wa Tuareg wamedai kuteka kambi mbili za jeshi Kaskazini mwa nchi

Nairobi – Waasi wa Tuareg kutoka Kaskazini mwa nchi ya Mali, wanasema wamechukua udhibiti wa kambi mbili za jeshi la serikali katikati mwa taifa hilo, hatua inayokuja wakati huu wasiwasi kati yao na utawala wa kijeshi ukiendelea ukiongezeka.

Msemaji wa waasi hao wa Tuareg amethibitisha kuchukua uongozi wa kambi mbili za kijeshi ambapo pia kundi hilo maarufu kama CMA limedai kuangusha ndege ya kijeshi
Msemaji wa waasi hao wa Tuareg amethibitisha kuchukua uongozi wa kambi mbili za kijeshi ambapo pia kundi hilo maarufu kama CMA limedai kuangusha ndege ya kijeshi AFP - SOULEYMANE AG ANARA
Matangazo ya kibiashara

Afisa wa serikali ya Mali amesema kulikuwepo na vifo vilivyotokana na shambulio hilo la Jumapili katika mji wa Léré katika eneo la Timbuktu japokuwa hakuweza wazi ni watu wangapi waliuawa.

Mkataba wa amani kati ya waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga uliotiwa saini mwaka wa 2015 umekuwa ukiyumba tangu kuondolewa kwa utawala wa kiraia mwaka wa 2020.

Hatua ya mamlaka ya kijeshi nchini Mali kuwafukuza walinda amani wa Umoja wa mataifa kwenye taifa hilo mwezi uliopita imechangia kuongezeka kwa mzozo.

Mzozo huo mpya na waasi wa Tuareg unakuja wiki kadhaa baada ya kundi la (GSIM) linahusishwa na  Al-Qaeda kusema kuwa linatangaza "vita katika eneo la Timbuktu
Mzozo huo mpya na waasi wa Tuareg unakuja wiki kadhaa baada ya kundi la (GSIM) linahusishwa na  Al-Qaeda kusema kuwa linatangaza "vita katika eneo la Timbuktu © Soumeylane Ag Anara / AFP

Msemaji wa waasi hao wa Tuareg amethibitisha kuchukua uongozi wa kambi mbili za kijeshi ambapo pia kundi hilo maarufu kama CMA limedai kuangusha ndege ya kijeshi.

Siku chache kabla,  muungano  wa waasi hao ulikuwa umetangaza kuanza tena makabiliano na serikali ambapo siku ya Jumanne ulipambana na wanajeshi wa serikali katika mji wa Bourem na kusababisha vifo kutoka pande zote mbili.

Viongozi wa kijeshi wa Niger, Burkina Faso na Mali walitia saini makubaliano ya pamoja ya ulinzi mjini Bamako mwishoni mwa juma
Viongozi wa kijeshi wa Niger, Burkina Faso na Mali walitia saini makubaliano ya pamoja ya ulinzi mjini Bamako mwishoni mwa juma © AFPTV

Mzozo huo mpya na waasi wa Tuareg unakuja wiki kadhaa baada ya kundi la (GSIM) linahusishwa na  Al-Qaeda kusema kuwa linatangaza "vita katika eneo la Timbuktu".

Viongozi wa kijeshi wa Niger, Burkina Faso na Mali walitia saini makubaliano ya pamoja ya ulinzi mjini Bamako mwishoni mwa juma, ambapo waliahidi kusaidiana iwapo wangeshambuliwa na vikosi vya kigeni au maasi ya ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.