Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Mazishi ya Chifu wa Wazulu Mangosuthu Buthelezi yanafanyika

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa waombolezaji wanaohudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe nchini humo na chifu wa Wazulu Mangosuthu Buthelezi, katika mji wa Ulundi.

Jeneza la Mangosuthu Buthelezi, mwana mfalme, kiongozi wa chama na Waziri Mkuu wa kimila, likiwa limebebwa wakati wa mazishi yake, Ulundi, Afrika Kusini, Jumamosi hii, Septemba 16, 2023.
Jeneza la Mangosuthu Buthelezi, mwana mfalme, kiongozi wa chama na Waziri Mkuu wa kimila, likiwa limebebwa wakati wa mazishi yake, Ulundi, Afrika Kusini, Jumamosi hii, Septemba 16, 2023. AFP - MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa zamani amepewa mazishi ya kitaifa kutokana na mchango wake katika vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.

Kifo cha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 95 kimezua mjadala kuhusu suala la urithi wake

Buthelezi alizaliwa katika familia ya kifalme ya Wazulu, ambapo alikuwa waziri mkuu wao hadi kifo chake.

Buthelezi alizaliwa katika familia ya kifalme ya Wazulu, ambapo alikuwa waziri mkuu wao hadi kifo chake
Buthelezi alizaliwa katika familia ya kifalme ya Wazulu, ambapo alikuwa waziri mkuu wao hadi kifo chake © Cyril Ramaphosa

Alianzisha chama cha Zulu cha Inkatha Freedom Party (IFP) baada ya kukatishwa tamaa na chama cha African National Congress (ANC) mwaka wa 1975 katika kilele cha utawala wa kibaguzi.

Chifu huyo pia alipinga msimamo wa ANC kuhusu hatua za kutumia silaha na vikwazo, akisema kuwa viliwadhuru raia wa Afrika Kusini weusi.

Rais Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa wale wanaohudhuria mazishi hayo
Rais Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa wale wanaohudhuria mazishi hayo © Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, alitangaza kuperushwa kwa bendera nusu mlingoti kote nchini humo kwa heshima ya kiongozi huyo.

Kwa upande mwengine kampuni ya kitaifa ya umeme pia imekubali, eneo la Ulundi halitakabiliwa na mgao wa umeme kitaifa wakati wa mazishi yake kama njia moja ya kutoa heshima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.