Pata taarifa kuu

Morocco: Baada ya tetemeko la ardhi, changamoto za ujenzi mpya

Wiki moja baada ya tetemeko la ardhi lililokumba nchi ya Morocco, na kuua watu 2,946 na kuwaacha zaidi ya watu 15,000 bila makazi na kuharibu makumi ya maelfu ya nyumba, Morocco tayari inafikiria siku cha kufanya baada ya janga hili.

Kijiji cha Imi N'Tala, kilichoharibiwa na tetemeko la ardhi, Septemba 14, 2023.
Kijiji cha Imi N'Tala, kilichoharibiwa na tetemeko la ardhi, Septemba 14, 2023. REUTERS - NACHO DOCE
Matangazo ya kibiashara

Vipi mwaka wa shule utaanza wakati shule 500 zilibomoka? Na juu ya yote, ujenzi utasimamiwa vipi baada ya tetemeko baya la ardhi lililotokea wiki moja iliyopita? Haya ndiyo maswali ambayo mamlaka na wasanifu majengo wa Morocco wanajiuliza leo. Kwanza, kunatakiwa kuchunguza hali hiyo.

Kwenye sitaha kuanzia Jumamosi asubuhi, wasanifu majengo watashiriki katika ukaguzi wa majengo yote, anaripoti mwandishi wetu wa Morocco, Seddik Khalfi. Jawad el-Basri ni mkuu wa chama cha wasanifu Majengo huko Marrakech: "Tumefungua orodha, tuna mamia ya wasanifu wa kujitolea," anaeleza.

Majengo ya pamoja

Kwa ujenzi upya, kipaumbele kinatolewa kwa vifaa vya jamii: shule, misikiti na zahanati lazima zianze tena haraka iwezekanavyo. "Huko Marrakech pekee, kuna shule 86 ambazo zimeathiriwa," anasema. Tunaunda tume kuhusiana na vifaa hivi vya kijamii. Huu ni uratibu wa kipekee. Tumeweka juhudi pamoja na tumekubaliana kutogawanyika. "

Barabara nyingi zilifungwa baada ya mawe na udongo kuprpmokea barbarani, kama hapa karibu na mji wa Adassil,Septemba 11, 2023.
Barabara nyingi zilifungwa baada ya mawe na udongo kuprpmokea barbarani, kama hapa karibu na mji wa Adassil,Septemba 11, 2023. REUTERS - NACHO DOCE

Wasanifu majengo wanafanya kampeni ya muundo jumuishi. Wanasema hawafikirii kurudia makosa ya zamani. "Tumeomba mamlaka ya umma kufanya kazi kwa dharura, lakini sio kwa haraka, ili kuwe na muundo maalum wa usanifu wa miji," amebaini mmoja wa wasanifu. Tunaomba mamlaka za umma zinazoenda kujenga upya eneo hili ziwe na mradi jumuishi. » Wasanifu wa majengo wanatarajia kuwa na manufaa na kuboresha maisha ya kila siku ya wananchi wenzao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.