Pata taarifa kuu

Tetemeko la ardhi nchini Morocco: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 2,862

Idadi ya vifo vya muda kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo la kusini-magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech nchini Morocco siku ya Ijumaa imeongezeka hadi vifo 2,862, Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza hivi punde Jumatatu usiku.

Mtu huyu akipita katika jengo lililodondoka kutokana na tetemeko la ardhi katika kijiji cha Tafeghaghte, karibu na Marrakech, Morocco, Jumatatu Septemba 11, 2023.
Mtu huyu akipita katika jengo lililodondoka kutokana na tetemeko la ardhi katika kijiji cha Tafeghaghte, karibu na Marrakech, Morocco, Jumatatu Septemba 11, 2023. AP - Mosa'ab Elshamy
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo pia limesababisha majeruhi 2,501 kwa mujibu wa chanzo hicho. Ripoti ya awali iliyochapishwa mapema Jumatatu iliripoti vifo vya watu 2,497 na 2,476 kujeruhiwa.

Tetemeko la ardhi, ambalo ndilo baya zaidi katika nchi hiyo ya kifalme kwa zaidi ya miaka sitini, liliharibu vijiji vizima Ijumaa jioni katika eneo lililo kusini magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech, katikatimwa nchi, na kusababisha vifo vya watu 2,681 na 2,501 kujeruhiwa, kulingana na ripoti rasmi ya hivi karibuni iliyochapishwa siku ya Jumatatu jioni.

Siku ya Jumapili jioni, Morocco ilitangaza kuwa imekubali ombi kutoka nchi nne kutuma timu za utafutaji na uokoaji: Uhispania, Uingereza, Qatar na Falme za Kiarabu.

Kulingana na waandishi wa shirika la habari la AFP, waokoaji wa Uhispania wako katika maeneo mawili yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi kusini mwa Marrakech, Talat Nyaqoub na Amizmiz.

"Ugumu mkubwa uko katika maeneo ya mbali na kuna ugumu wa kufika katika maeneo hayo kama hapa, lakini waliojeruhiwa wanasafirishwa kwa ndege," mkuu wa timu kutoka Uhispania, Annika Coll, ameliiambia shirika la habari la AFP.

Tetemeko la ardhi lilifikia kipimo cha 7 kulingana na Kituo cha Morocco cha Utafiti wa Sayansi na Ufundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.