Pata taarifa kuu

Morocco: Zoezi la kuwatafuta manusura lashika kasi baada ya tetemeko kubwa la ardhi

Waokoaji wameendelea na zoezi la kujaribu kutafuta manusura waliokwama chini ya vifusi katika vijiji vilivyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 kusini magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech.

Tetemeko la ardhi lililotokea Ijumaa jioni, la kipimo cha 7 kulingana na Kituo cha Morocco cha Utafiti wa Sayansi na Kiufundi, ndilo tetemeko lenye nguvu zaidi kuwahi kupiga nchini Morocco.
Tetemeko la ardhi lililotokea Ijumaa jioni, la kipimo cha 7 kulingana na Kituo cha Morocco cha Utafiti wa Sayansi na Kiufundi, ndilo tetemeko lenye nguvu zaidi kuwahi kupiga nchini Morocco. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika eneo hilo, tetemeko la ardhi la nyuzi 4.5 kwenye kipimo cha Richter lilipiga siku ya Jumapili, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Jiofizikia nchini Morocco (ING).

Waokoaji, watu waliojitolea na wanajeshi wanafanya kazi ya kutafuta manusura na kutoa miili kutoka kwa vifusi, hasa katika kijiji cha Tafeghaghte, lililoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi, kitovu chake ambacho kiko umbali wa kilomita hamsini tu , kulingana na timu ya waandishi wa habari wa shirika la Habari laAFP. Majengo machache bado yamesimama.

Waokoaji wameweza kutoa mwili kutoka kwa nyumba iliyoharibiwa. Lakini miili mingine minne bado imekwama chini ya vifusi, kulingana na wakaazi.

"Watu wote wameangamia, moyo wangu unauma, siwezi kufarijiwa" anaangua kilio, Zahra Benbrik, 62, ambaye anadai kuwa amepoteza wapendwa wake 18.

"Mwili wa kaka yangu ndio umebaki chini ya vifusi, siwezi kusubiri wamtoe ili niomboleze kwa amani," amebaini.

Msaada wa kimataifa

Huko Marrakech, jiji lililo katikati mwa Morocco, wakaazi wengi wamekimbilia hospitali kutoa damu kwa waathiriwa.

"Inapendeza sana kuona haya yote kutoka kwa raia, na hata wageni ambao hawana uhusiano wowote na hali hii hapa walikuja kuchangia damu," amesema Youssef Qornafa, mwanafunzi aliyechangia damu katika kituo cha kuongezewa damu.

Tetemeko la ardhi lililotokea Ijumaa jioni, likiwa na kipimo cha 7 kulingana na Kituo cha Morocco cha Utafiti wa Sayansi na Kiufundi (6.8 kulingana na shirika la Seismological la Marekani), ndilo lenye nguvu zaidi kuwahi kupiga nchini Morocco.

Tetemeko hili limesababisha vifo vya watu 2,122 na 2,421 kujeruhiwa, ambao 1,404 wako katika hali mbaya, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza siku ya Jumamosi jioni, idadi ya watu ambayo inaweza kuongezeka wakati zoezi la kutafuta miili likiendelea.

Mkoa wa Al-Haous, ambapo kukapatikana kitovu cha tetemeko la ardhi, ndio uliopoteza zaidi watu 1,293, ukifuatiwa na mkoa wa Taroudant wenye vifo 452. Katika maeneo haya mawili yaliyo kusini-magharibi mwa Marrakech, vijiji vizima viliathiriwa.

Maombolezo ya kitaifa ya siku tatu yalitangazwa siku ya Jumamosi. Bendera kwenye majengo ya serikali zimepandishwa nusu mlingoti.

Nchi nyingi zikiwemo Marekani, Uingereza na Italia zimetoa msaada. Hata nchi jirani ya Algeria, yenye uhusiano tata na Morocco, imefungua anga yake, iliyofungwa kwa miaka miwili, kwa ndege za kusafirisha misaada na majeruhi.

Uhispania ilituma timu ya waokoaji 56 nchini Morocco baada ya kupokea ombi rasmi la usaidizi kutoka Rabat.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema nchi yake iko tayari "kuingilia kati" kusaidia Morocco wakati mamlaka ya Morocco "itaona kuwa ni muhimu."

Israeli, ambayo ilifufua uhusiano wake na Morocco mnamo 2020, ilijitolea kutuma timu za uokoaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.