Pata taarifa kuu

Watu 300 waangamia kutokana na tetemeko la ardhi nchini Morocco

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo cha Richter limepiga katikati mwa Morocco, katika eneo la Marrakech, usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi. Tetemeko hili limesababisha vifo na uharibifu mkubwa. Idadi ya wahanga inaongezeka kila wakati.

Moja ya picha za kwanza (televisheni ya Morocco) zilizopigwa mjini Marrakech, muda mfupi baada ya tetemeko la ardhi lililotikisa jiji hilo na jimbo lake, usiku wa Septemba 9, 2023.
Moja ya picha za kwanza (televisheni ya Morocco) zilizopigwa mjini Marrakech, muda mfupi baada ya tetemeko la ardhi lililotikisa jiji hilo na jimbo lake, usiku wa Septemba 9, 2023. via REUTERS - AL OULA TV
Matangazo ya kibiashara

Kitovu cha tetemeko hili la ardhi kinapatikana kusini magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech, kilomita 320 kusini mwa mji mkuu Rabat. Kulingana na Taasisi ya Marekani ya Jiofizikia (USGS). Kituo cha Kitaifa cha Utafiti wa Sayansi na Kiufundi (CNRST) chenye makao yake mjini Rabat, kwa upande wake, kimebainisha kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa nyuzi 7 kwenye vipimo vya Richter na kwamba kitovu chake kilikuwa katika mkoa wa Al- Haousi.

Kulingana na vyombo vya habari vya Morocco, hili ndilo tetemeko la ardhi lenye nguvu zaidi kuwahi kukumba nchi ya Morocco hadi sasa. "Kulingana na ripoti ya hivi punde, tetemeko hili la ardhi limesababisha vifo vya watu 296 katika majimbo na wilaya za al-Haous, Marrakech, Ouarzazate, Azilal, Chichaoua na Taroudant," wizara imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. Watu 153 wamejeruhiwa na kulazwa hospitalini, kulingana na chanzo kimoja. Ikinukuu vyanzo vya matibabu, tovuti ya habari ya Médias24 imeripoti "idadi kubwa" ya watu waliojeruhiwa wamesafirishwa katika hospitali za Marrakech.

Video zilianza kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii, nyingi zilirekodiwa huko Marrakech na jimbo lake. Zinaonyesha kukatika kwa umeme kwa ghafla, wakati huo uo watu wanaonekana kuwa na hofu, huku huduma ya kwanza kwa waathiriwa ikitolewa kati ya maporomoko ya ardhi na vifusi. Msikiti katika uwanja maarufu wa Jamaâ El Fnaa pia umeathirika.

(Pamoja na mashirika)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.