Pata taarifa kuu

Morocco: Aliyemkosoa mfalme amefungwa jela miaka mitano

Nairobi – Wakili wa raia wa Morocco anayetuhumiwa kwa makosa ya kumkosoa mfalme wa taifa hilo kwenye mitandao ya kijamii, amewaambia waandishi wa habari kwamba mteja wake amefungwa jela miaka mitano.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo kifungu cha Boukioud 267-5, mtu anaweza fungwa jela kati ya miezi sita na miaka miwili kwa makosa ya kudharau ufalme
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo kifungu cha Boukioud 267-5, mtu anaweza fungwa jela kati ya miezi sita na miaka miwili kwa makosa ya kudharau ufalme AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Said Boukioud alishtakiwa kwa tuhuma za kudhalilisha ufalme kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa facebook mwaka wa 2020 kukosoa hatua ya Morocco kurejesha uhusiano na Israeli wakati huo akiishi nchini Qatar.

Boukioud alifuta chapisho hilo na baadae kufuta akaunti yake ya facebook baada ya kubaini kwamba alikuwa ameshtakiwa nchini Morocco.

Kwa mujibu wa katiba ya Morocco, masula ya kigeni ni majukumu ya mfalme na kwamba matamshi yoyote yanayoonekana kukosoa mamlaka ya mfalme yanaadhibiwa vikali.

Wakili wa raia huyo wa Morocco El Hassan Essouni, ametaja hukumu hiyo kama kali na isiyooelezeka na kwamba mteja wake atakata rufa.

Mfalme wa Morocco Mohammed VI, amesema nchi yake itatumia Dolla Bilioni 11.6 kwa ajili ya kujenga upya maeneo yalioharibiwa baada ya tetemeko la ardhi
Mfalme wa Morocco Mohammed VI, amesema nchi yake itatumia Dolla Bilioni 11.6 kwa ajili ya kujenga upya maeneo yalioharibiwa baada ya tetemeko la ardhi © MOROCCAN AGENCY PRESS / AFP

Taarifa ya wakili huyo imeeleza kwamba licha mteja wake kukosoa ushirikiano kati ya nchi yake na Israeli, hakuwa na nia ya kumuudhi mfalme.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo kifungu cha Boukioud 267-5, mtu anaweza fungwa jela kati ya miezi sita na miaka miwili kwa makosa ya kudharau ufalme.

Kifungo hicho kinaweza kuongezwa kwa miaka mitano iwapo kosa limefanyika hadharani pamoja na kutumia mifumo ya kielekitroniki kusambza.

Watetezi wa haki za binadamu nchini humo wanasema sheria hiyo inaminya uhuru wa watu kujieleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.