Pata taarifa kuu

Ulimwengu wasaidia Morocco baada ya tetemeko la ardhi lililoua zaidi ya watu 2,000

Kuanzia Ufaransa hadi Marekani, kupitia Israel, nchi mbalimbali duniani zimetoa msaada wao kwa Morocco, iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000.

Waokoaji wameendelea na zoezi la kujaribu kutafuta manusura waliokwama chini ya vifusi katika vijiji vilivyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 kusini magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech.
Waokoaji wameendelea na zoezi la kujaribu kutafuta manusura waliokwama chini ya vifusi katika vijiji vilivyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 kusini magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech. AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Waokoaji wameendelea na zoezi la kujaribu kutafuta manusura waliokwama chini ya vifusi katika vijiji vilivyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 kusini magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakech.

Katika eneo hilo, tetemeko la ardhi la nyuzi 4.5 kwenye kipimo cha Richter lilipiga tena siku ya Jumapili, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Jiofizikia nchini Morocco (ING).

MAREKANI

Naibu Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jon Finer amesema nchi yake "imeiambia serikali ya Morocco kwamba iko tayari kutoa msaada muhimu." "Tuna timu za utafutaji na uokoaji zilizo tayari kutuma wafanyakazi wake" na "pia tuko tayari kutoa fedha kwa wakati ufaao ili kuwasaidia Wamorocco wasiweze kukata tamaa na kukabiliana na janga hili la kutisha," amesema.

ULAYA

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye alizungumzia "janga ambalo linatuathiri sisi sote", alionyesha kuwa Paris "imekusanya timu zote za kiufundi na usalama ili kuweza kuingilia kati wakati mamlaka ya Morocco itaona kuwa ni muhimu".

Timu ya wazima moto wa kujitolea wa Ufaransa kutoka eneo la Lyon (katikati-mashariki) tayari wamewasili Morocco siku ya Jumapili na watashiriki katika shughuli za uokoaji karibu kilomita hamsini kutoka Marrakech, kulingana na mamlaka ya mkoa huo. 

Uhispania imetangaza kuwa ilituma timu ya waokoaji 56 nchini Morocco siku ya Jumapili, baada ya kupokea ombi rasmi la usaidizi kutoka Rabat. Ndege ya kijeshi ya A400 iliruka kutoka kambi ya Zaragoza (kaskazini-mashariki) ikiwa na timu ya waokoaji kuelekea Marrakech "kusaidia katika utafutaji na uokoaji wa manusura", imesema Wizara ya Ulinzi ya Uhispania.

Kitovu cha tetemeko hili la ardhi, la ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo cha Richter kulingana na Taasisi ya Marekani ya Jiofizikia (USGS), kinapatikana kusini magharibi mwa Marrakech, kilomita 320 kusini mwa mji mkuu Rabat.

Uswisi ilijitolea kutoa makazi ya muda, vifaa vya kutibu na usambazaji wa maji, vifaa vya usafi wa mazingira na vifaa vya usafi. Uwasilishaji wa vifaa hivi utaambatana na wataalam kutoka Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Uswisi (CSA). Wizara ya Mambo ya Nje ya Uswizi ilisema Jumamosi jioni kwamba ilikuwa bado haijapata jibu la pendekezo hili.

Ulinzi wa Ubelgiji ulitangaza Jumamosi kuwa huduma ya uratibu wa misaada ya dharura nje ya nchi (B-Fast) ilianzishwa ili kujibu maombi ya usaidizi kutoka kwa mamlaka ya Morocco. 

Italia ilitoa msaada kutoka kwa kikosi chake cha ulinzi wa raia na wazima moto, huku Kanisa Katoliki la Italia likituma euro 300,000 kupitia shirika la Caritas Italia.

Rais wa Italia Sergio Mattarella Jumamosi alisisitiza "utayari wa Italia kuchangia kazi ngumu ya uokoaji."

Uturuki ilipendekeza siku ya Jumamosi kutumwa kwa waokoaji 265 na mahema 1,000, bila majibu kutoka mamlaka ya Morocco.

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amebaini kuwa nchi yake "iko tayari kutoa usaidizi unaohitajika, ikiwa ni pamoja na timu ya uokoaji".

MASHARIKI YA KATI

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza kwamba "Nchi ya Israel itatoa msaada wowote unaowezekana kwa Morocco, ikiwa ni pamoja na timu ya utafutaji na uokoaji, ikiwa ithitaji hilo."

Mwenzake wa Iraq Mohamed Chia al-Soudani pia amesema yuko "tayari kutoa msaada wa aina yoyote". Naye Mfalme Abdullah II wa Jordan ameagiza serikali yake "kutoa msaada wote unaohitajika kwa Morocco."

Qatar ilikuwa imetangaza kwamba timu ya uokoaji ingeondoka Doha Jumamosi jioni.

MASHIRIKA

Bw. Macron, mwishoni mwa mkutano wa G20 huko New Delhi, alitia saini na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, rais wa Comoro Azali Assoumani ambaye sasa anaongoza Umoja wa Afrika, na viongozi wa Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa na Tume ya Ulaya tamko la pamoja linaloahidi "kutoa msaada wote muhimu kwa mahitaji ya haraka ya muda mfupi na juhudi za ujenzi upya".

Shirikisho la Kimataifa la mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu lenye makao yake Geneva limetoa faranga milioni moja za Uswisi (dola milioni 1.1) kutoka kwa Hazina yake ya Kukabiliana na Maafa ya Dharura ili kusaidia kazi ya Hilali Nyekundu ya Morocco katika shughuli ya utafutaji na uokoaji.

Siku ya Jumamosi Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lilionya juu ya umuhimu wa mahitaji ya baadaye ya Morocco.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.