Pata taarifa kuu

Niger: Paris yataka 'kuachiliwa mara moja' kwa Mfaransa aliyekamatwa

Ufaransa imetangaza siku ya Jumanne kukamatwa kwa Stéphane Jullien, mshauri wa raia wa Ufaransa wanaoishi nje ya nchi walioko Niger Septemba 8 na vikosi vya usalama vya Niger, na kuomba "kuachiliwa kwake mara moja" na "bila masharti". 

Waandamanaji waliondoa bango la ubalozi wa Ufaransa nchini Niger, Julai 30, 2023.
Waandamanaji waliondoa bango la ubalozi wa Ufaransa nchini Niger, Julai 30, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Stéphane Jullien, mshauri wa raia wa Ufaransa nje ya nchi, alikamatwa mnamo Septemba 8 na vikosi vya usalama vya Niger.

"Ufaransa inatoa wito wa kuachiliwa kwake mara moja. Tangu siku ya kwanza, ubalozi wetu umehamasishwa kikamilifu ili kuhakikisha ulinzi wa kibalozi kwa raia wetu, "kulingana na taarifa kutoka kwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa.

Mshauri kwa Wafaransa walio ng'ambo anawakilisha raia wenzake walio nje ya nchi ya nchi katika balozi na balozi ndogo. Tangazo la kukamatwa kwa Stéphane Jullien linakuja katika hali ya wasiwasi mkubwa kati ya Paris na Niamey, tangu mapinduzi ya kijeshi ya Julai 26 nchini Niger.

Balozi wa Ufaransa atakiwa kuondoka

Ufaransa bado inamchukulia rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum, anayeshikiliwa na jeshi la serikali, kama mkuu halali wa nchi, na hadi sasa imekataa kujibu matakwa ya wanajrshi waliofanya mapinduzi. Utawala wa kijeqhi nchini Niger unadai kuondoka kwa balozi wa Ufaransa huko Niamey na walishutumu mikataba ya ulinzi na Paris, ambayo inapeleka wanajeshi 1,500 nchini Niger, nchi ambayo ilikuwa moja ya washirika wake wa mwisho katika ukanda wa Sahel kabla ya mapinduzi ya kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.