Pata taarifa kuu

Niger: Mvutano mpya waibuka kati ya Ufaransa na utawala wa kijeshi wa Niamey

Mvutano mpya umeibuka kati ya Paris na Niamey. Kutoka New Delhi, kando ya mkutano wa kilele wa G20, Rais Macron aliwajibu viongozi wa mapinduzi wa Niger, ambao kwa mara nyingine waliishutumu Ufaransa kwa kupanga uvamizi dhidi ya nchi yao.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa G20, mjini New Delhi, Jumapili hii, Septemba 10, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa G20, mjini New Delhi, Jumapili hii, Septemba 10, 2023. AP - Manish Swarup
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi, utawala wa kijeshi wa Niger, uliotokana na mapinduzi ya mwezi Julai, ambao uliishutumu Ufaransa kwa "kupeleka vikosi vyake" katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi, hususan Benin, Cote d'Ivoire na Senegal, kwa lengo la "kuivamia" Niger. "Luteka hizi" zinalenga "kufanikiwa kwa uingiliaji wa kijeshi dhidi ya nchi yetu," unasema utawala wa kijeshi wa Niamey.

Jibu kutoka Paris halikuchukua muda mrefu siku ya Jumapili. "Hatutambui uhalali wowote katika taarifa za utawala wa kijshi," rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kilele wa G20 nchini India.

"Vikosi vya Ufaransa viliwekwa katika ardhi ya Niger kwa ombi la Niger. Na tuko hapa kupambana na ugaidi kwa ombi la Niger na mamlaka yake iliyochaguliwa kidemokrasia, yaani Rais Bazoum, serikali yake na Bunge lake. Pia tumekuwa na hatua madhubuti ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa mashambulizi ya kigaidi katika ardhi ya Niger. Na tulifanya hivyo kwa gharama ya maisha ya wanajeshi kadhaa wa Ufaransa. Mapinduzi ya kijeshi tangu mwezi Julai mwaka huu yanamshikilia rais aliyechaguliwa kidemokrasia. Ufaransa ina msimamo rahisi: tunalaani, tunataka kuachiliwa kwa rais Bazoum na kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba. Na hatutambui uhalali wowote katika taarifa za utawala wa kijeshi. Kwa vile rais Bazoum hajaachia madaraka, ikiwa tutapeleka tena kitu chochote, tutafanya hivyo tu kwa ombi la rais Bazoum, na kwa uratibu naye. Sio na maafisa ambao, leo, wanamchukua rais mateka. Kuhusu suala hili, tangu siku ya kwanza, Ufaransa imekuwa ikishirikiana na marais wote wa kanda, wakuu wa nchi na serikali, na tunaunga mkono kikamilifu misimamo ya ECOWAS. ECOWAS ililaani hali hii, ilichukua vikwazo, kama vile UMOA, na ECOWAS inaendelea na kazi ya kutaka kuachiliwa Rais Bazoum na kuruhusu suala hili kutatuliwa. Ufaransa iko upande wa ECOWAS na inaiunga mkono. Kwa yaliyosalia sina nia maadamu hali iko hivi, kwa namna fulani inafungia kila kitu, kwa vile mtu pekee ambaye tunapaswa kuzungumza naye kihalali ni rais Bazoum. "

Wakati huo huo, hali ya Niger pia ilikuwa kiini cha majadiliano kati ya rais wa Urusi Vladimir Putin na mkuu wa mpito nchini Mali, Assimi Goïta. Mazungumzo ya simu "kwa jitihada za upande wa Mali", imebaini Kremlin katika taarifa kwa vyombo vya habari. Viongozi wote wawili wameitangaza kuunga mkono suluhu la kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.