Pata taarifa kuu

Niger: Utawala wa kijeshi washutumu makubaliano ya kijeshi na Ufaransa

Wakati ujumbe kutoka ECOWAS uliwasili Niamey kuanzisha mazungumzo na wanajeshi waliochukua mamlaka nchini Niger, wajumbe hao walichukua hatua na misimamo mikali Alhamisi jioni Agosti 3. Utawala wa kijeshi umelaani mikataba ya kijeshi iliyohitimishwa na Ufaransa, kuwaondoa mabalozi kutoka nchi nne na kutangaza kwamba itajibu "uchokozi wowote" kutoka ECOWAS.

Picha iliyopigwa kutoka video ya ORTN - Télé Sahel mnamo Julai 31, 2023 ikimuonyesha Kanali-Meja Amadou Abdramane akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa.
Picha iliyopigwa kutoka video ya ORTN - Télé Sahel mnamo Julai 31, 2023 ikimuonyesha Kanali-Meja Amadou Abdramane akisoma taarifa kwenye televisheni ya taifa. © AFP -
Matangazo ya kibiashara

Hali bado ni ya wasiwasi nchini Niger, zaidi ya wiki moja baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Baraza la Ulinzi wa Kitaifa (CNSP), ambalo sasa liko madarakani. Mapema jioni ya Agosti 3, wajumbe kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) waliwasili Niamey, kwa lengo la kuanzisha mazungumzo na viongozi wa mapinduzi ili kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba. Mazungmzo ya kwanza yalikwenda vizuri.

Lakini usiku, CNSP ilizungumza kupitia sauti ya Kanali-Meja Amadou Abdramane, yuleyule aliyezungumza Julai 26, wakati wanajeshi walipotangaza kuwa wamempindua Rais Mohamed Bazoum. Viongozi wa mapinduzi nchini Niger walichukua msimamo katika masuala matatu.

Viongozi wa mapinduzi walaani "mikataba ya ushirikiano katika sekta ya usalama na ulinzi" na Ufaransa

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, wameshutumu mikataba kadhaa ya kijeshi iliyohitimishwa na Ufaransa, ambayo inahusu hasa "kupiga kambi" kwa kikosi cha Ufaransa na "hadhi" ya askari waliopo ndani ya mfumo wa mapambano dhidi ya wanajihadi. "Kutokana na mtazamo usio kuwa wa kawaida wa Ufaransa na hatua za Ufaransa kwa hali inaojiri " nchini Niger, "Baraza la Ulinzi wa Kitaifa linaamua kushutumu mikataba ya ushirikiano katika nyanja ya usalama na ulinzi na nchi hii," Amadou Abdramane amesema.

Ufaransa iliwaondoa raia wake 577 kutoka Niger mnamo Agosti 1 na 2, kutokana na hali mbaya nchini humo. Uamuzi ulioshutumiwa na mamlaka ya kijeshi. Aidha, Ufaransa ina wanajeshi 1,500 waliotumwa nchini Niger kama sehemu ya mapambano dhidi ya ugaidi.

Wanajeshi hao pia waliamua "kusitisha shughuli za mabalozi wa Jamhuri ya Niger" katika nchi nne: Ufaransa na Marekani, washirika wawili wa Rais Bazoum, Nigeria, ambaye Rais wake Bola Tinubu pia yni rais wa ECOWAS na ambayo iliweka vikwazo dhidi ya Niger - kusitishwa kwa miamala ya kifedha na kibiashara, kuzuia mali ya viongozi wa mapinduzi, kukata usambazaji wa umeme... -, na Togo.

Hatimaye, viongozi wa mapinduzi nchini Niger wametoa onyo kwa ECOWAS, ambayo ilitoa makataa hadi Agosti 6 kwa ajili ya kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba, bila hivyo itaingilia kati kijeshi. "Uchokozi wowote au jaribio la uchokozi dhidi ya Niger litakabiliana na jibu kutoka kwa vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Niger, isipokuwa nchi marafiki zilizosimamishwa kwa uanachama wa jumuiya hiyo", walionya askari hao.

"Nchi hizi rafiki" zilizosimamishwa kwenye uanachama wa ECOWAS ni Burkina Faso na Mali, pia zikiongozwa na wanajeshi katika mshikamano na mapinduzi ya wiki iliyopita na tayari kushirikiana na nguvu mpya huko Niamey. Jenerali Salifou Mody, nambari mbili wa CNSP, pia alizuru Ouagadougou mnamo Agosti 2 na 3.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.