Pata taarifa kuu

Niger: Ufaransa yatangaza rasmi kumalizika kwa operesheni yake ya kuwahamisha raia

"Zoezi la kuwahamisha raia wetu kutoka Niger limekamilika" na "Wafaransa na raia kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya 1,079 sasa wako salama", amesema Waziri wa Majeshi ya Ufaransa, Sébastien Lecornu, kwenye mtandao wa kijamii wa X mnamo Agosti 3, 2023.

Watu wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Paris-Charles-de-Gaulle huko Roissy-en-France, karibu na Paris, mnamo Agosti 2, 2023, baada ya kuhamishwa kutoka Niger.
Watu wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Paris-Charles-de-Gaulle huko Roissy-en-France, karibu na Paris, mnamo Agosti 2, 2023, baada ya kuhamishwa kutoka Niger. AFP - LOU BENOIST
Matangazo ya kibiashara

Agosti 1, 2023. mamlaka ya Ufaransa ilianzisha operesheni ya kuwahamisha raia wake kwa hiari iliyo wazi na wale wa nchi nyingine. Operesheni ilifanyika kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini Niger mnamo Julai 26 na "vurugu" wakati wa maandamano mbele ya ubalozi wa Ufaransa huko Niamey mnamo Julai 30.

Tangazo lililothibitishwa Alhamisi hii na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, na rais mwenye Emmanuel Macron katika ukurasa wake wa Twitter.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa inabaini kwamba "zoezi la kuwahamisha raia sasa limekamilika". Quai d'Orsay inabainisha kuwa "Ufaransa imewahamisha watu 1,079: raia 577 wa Ufaransa, na raia kadhaa kutoka mataifa mengine mengi".

Miongoni mwa watu hawa waliohamishwa kutoka Niger, kuna raia wa Benin, Botswana, Cameroon, Cape Verde, Kongo, Ethiopia, Gabon, Ghana, Guinea, Côte d'Ivoire, Madagascar, Mali, Morocco, Mauritania, Nigeria, Senegal, Togo na Tunisia, miongoni mwa wengine.

Jumla ya ndege tano zimekodiwa na jeshi la Ufaransa tangu Jumanne. Uhamisho huu ulifanyika kwa hiari. Zoezi ambalo lilifanyika kwa takriban masaa 48. Takriban Wafaransa 600 wameelezea nia yao ya kuondoka nhini Niger. Jumla ya Wafaransa 1,200 wamesajiliwa kwenye orodha za ubalozi, lakini baadhi yao wako likizo nje ya Niger.

'Hakuna sababu madhubuti ya kuondoka Niger'

Tarehe 2 Agosti, wanadiplomasia wa Ufaransa kwa mara nyingine tena walilaani "vikali ghasia zilizofanywa dhidi ya ubalozi wake nchini Niger, Jumapili Julai 30, na makundi yaliyopangwa na yaliyojihami kwa silaha", na kuthibitisha kwamba "usalama wa majengo ya kidiplomasia na wafanyakazi ni wajibu chini ya sheria za kimataifa. , ikijumuisha Mikataba ya Vienna”.

Mnamo Agosti 2, Jenerali Abdourahamane Tchiani, mkuu wa Baraza la Ulinzi wa taifa (CNSP), chombo kilichompindua Rais Mohamed Bazoum, alisema kwamba raia wa kigeni waliopo katika ardhi ya Niger "hawajawahi kulengwa naa tishio hata kidogo" na kwamba "hawana sababu madhubuti ya kuondoka Niger", katika hotuba ya televisheni katika mkesha wa Siku ya Uhuru wa nchi hiyo, Agosti 3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.