Pata taarifa kuu

Mapinduzi Niger: Utawala wa kijeshi waishutumu Ufaransa kwa kuandaa 'uvamizi'

Utawala wa kijeshi wa Niger uliotokana na mapinduzi ya kijeshi umeishutumu Ufaransa kwa "kupeleka vikosi vyake" katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi kwa nia ya 'kuivamia' Niger.

Maelfu ya wananchi wa Niger waliandamana mbele ya kambi ya wanajeshi wa Ufaransa wakitaka waondoke nchini humo.
Maelfu ya wananchi wa Niger waliandamana mbele ya kambi ya wanajeshi wa Ufaransa wakitaka waondoke nchini humo. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

"Ufaransa inaendelea kupeleka vikosi vyake katika nchi kadhaa za ECOWAS (Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi) kama sehemu ya maandalizi ya uvamizi dhidi ya Niger, ambayo inapanga kwa kushirikiana na ECOWASa," amesema mmoja wa wajumbe wa utawala huo wa kijeshi, Kanali-Meja Amadou Abdramane, katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, utawala huo umebainisha tangu Septemba 1 kwamba "ndege mbili za kijeshi za aina ya A400M na Dornier 328 zimetumwa nchini Côte d'Ivoire", na kwamba "helikopta mbili za aina ya Super Puma" na "magari aidi ya arobaini ya kivita" yalikuwa "Kandi na Malanville nchini Benin".

Meli ya Ufaransa huko Benin

"Mnamo Septemba 7, 2023, meli ya kijeshi ya Ufaransa ilitia nanga Cotonou (Benin) ikiwa na wafanyakazi na vifaa vya kijeshi," kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Majenerali walio madarakani pia wanaripoti "takriban safari za ndege za kijeshi zaidi ya mia moja za mizigo zimewezesha kutua kwa kiasi kikubwa chavifaa na zana za kivita nchini Senegal, Côte d'Ivoire na Benin."

"Luteka hizi" hizi zinalenga "kufanikiwa katika uingiliaji wa kijeshi dhidi ya nchi yetu," kulingana na utawala wa kijeshi nchini Niger.

Tishio la uingiliaji kati wa ECOWAS

Baada ya mapinduzi ya Julai 26, ECOWAS ilitishia kuingilia kijeshi nchini Niger, ambayo ilikuwa imetangaza kujitayarisha, kurejesha utulivu wa kikatiba, kumwachilia huru rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum na kumrejesha mamlakani.

Uamuzi ulioungwa mkono na Ufaransa, ambayo ina takriban wanajeshi 1,500 katika nchi hii ya Sahel, kama sehemu ya mapambano dhidi ya wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.