Pata taarifa kuu

Makata ya ECOWAS nchini Niger: 'Chad haitaingilia kijeshi kamwe'

Niger bado imetumbukia karika sintofahamu. Makataa ya ECOWAS yatakwisha siku ya Jumapili Agosti 6. Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kiucjhumi ya Nchi za Afrika Magharibi zinajitayarisha kwa uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini humo. Kwa siku tatu na hadi jana, Ijumaa, wakuu wa majeshi kutoka ECOWAS walikuwa wakikutana Abuja, Nigeria, kufafanua mbinu za "kuingilia kati kijeshi."

Mkutano wa ECOWAS mjini Abuja, Nigeria mnamo Agosti 2, 2023 kujadili mapinduzi ya Niger.
Mkutano wa ECOWAS mjini Abuja, Nigeria mnamo Agosti 2, 2023 kujadili mapinduzi ya Niger. AFP - KOLA SULAIMON
Matangazo ya kibiashara

Inaonekana kuwa kikosi kiko tayari. Ni kikosi kinachosubiri, kilichoidhinishwa mwezi Desemba mwaka uliyopita, katika mkutano wa wakuu wa nchi wa ECOWAS. Kikosi kilichoundwa awali kwa ajili ya kulinda amani na mapambano dhidi ya ugaidi, lakini kwa upande wa Niger, askari hawa wanapaswa kuwa na mamlaka thabiti, kwa hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu, na vitendo vya mashambulizi vilivyoidhinishwa.

Kikosi hili kinapaswa kupitia ardhini, baharini na angani, ingawa, kulingana na mshiriki, shughuli za shamba zinaweza kulengwa mwanzoni.

Jumamosi hii, Agosti 5, kila Mkuu wa Majeshi aliyekuwepo Abuja atawasilisha mpango wa kuingilia kati kijeshi kwa rais wa nchi yake kwa sababu, itakumbukwa, Wakuu wa Nchi ndio watakaoamua kuanzisha operesheni hiyo.

Jukumu kuu la Nigeria

Kuhusu njia za kijeshi na idadi ya askari ambao wantaweza kutumwa, hii hapa ni katika masuala ya siri za ulinzi, kwa sasa. Hata hivyo, Nigeria inatarajiwa kuwa na jukumu kubwa katika operesheni hiyo na inaweza kuchukua usimamizi wa kikosi hiki cha kikanda.

Côte d'Ivoire pia itakuwa nguvu muhimu hata kama, kulingana na chanzo kizuri, "Abidjan inatumai hadi dakika ya mwisho kwa suluhu la kirafiki" na viongozi wa mapinduzi nchini Niger .

Benin na Senegal pia zitashiriki na orodha inaweza kuwa ndefu. Walakini, operesheni hii haiungwi mkono kwa kauli moja. Ingawa si si mwanachama wa  kanda ndogo, Chad inasema haitatuma askari yeyote nchini Niger.

'Chad haitaingilia kijeshi nchini Niger'

Chad, nchi yenye nguvu kubwa ya kijeshi barani Afrika na nchi jirani ya Niger, imesema kwamba haitashiriki katika uingiliaji kati wowote. "Chad haitaingilia kijeshi kamwe. Daima tumetetea mazungumzo. Chad ni mwezeshaji”, alitangaza, Ijumaa Agosti 4, Daoud Yaya Brahim, Waziri wa Majeshi ya Chad, nchi ambayo si mwanachama wa ECOWAS.

Algeria, pia, inapinga operesheni yoyote ya kijeshi. Ofisi yake ya Mambo ya Nje inaamini hilo lingekuwa chaguo la "bahati mbaya". Algiers yaonya na kutoa wito wa "tahadhari na vizuizi", kwani uingiliaji kati huu unaweza kutatiza na kuzidisha mzozo wa sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.