Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mali: Muungano wa waasi wa Azawad watangaza vita dhidi ya utawala wa kijeshi

Je, taifa la Mali linaelekea katika kipindi kipya cha uhasama na waasi wa zamani wa kaskazini mwa nchi hiyo? Katika taarifa kwa vyombo vya habari, muungano wa makundi ya zamani ya waasi ya Azawad (CMA) linatoa wito kwa wakaazi wa eneo hilo "kwenda kwenye uwanja wa vita kuchangia juhudi za vita" dhidi ya vikosi vya jeshi na washirika wao kutoka Urusi.

Wanajeshi wa Tuareg kutoka Vuguvugu la Kitaifa la Ukombozi wa Azawad, wanachama wa CMA, hapa wakati wakipiga doria katika mitaa ya Kidal mnamo Agosti 28, 2022.
Wanajeshi wa Tuareg kutoka Vuguvugu la Kitaifa la Ukombozi wa Azawad, wanachama wa CMA, hapa wakati wakipiga doria katika mitaa ya Kidal mnamo Agosti 28, 2022. © Soumeylane Ag Anara / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwishoni mwa mwezi Agosti, mapigano yamezuka tena kati ya jeshi la serikali na makundi kutoka kaskazini. Pande zote mbili zinashutumu kila mmoja kwa kuanzisha tena uhasama. Matukio ambayo yanazidi kutilia shaka makubaliano ya amani ya Algiers yaliyotiwa saini mnamo mwaka 2015.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Kanali Moulay Ag Sidi Mola, msemaji wa muungano wa makundi ya Azawad, anafuatilia mpangilio wa matukio ya hivi punde ambayo,yanachochea mzozo mpya.

Kuanzishwa kwa uhasama ambao unaonekana kutoepukika na ambao waasi wa zamani wanauhusisha na jeshi la Mali na mamluki wa Wagner.

CMA inatoa wito kwa "wakazi wote wa Azawad kwenda uwanjani kuchangia juhudi za vita kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya nchi na hivyo kurejesha udhibiti wa eneo lao lote".

Tamko hilo linathibitisha kwamba "jeshi la taifa la Azawadi" "limetayarisha mikakati ya muda mfupi na ya muda mrefu kwa lengo la kupambana vilivyo". Makundi ya waasi ya kaskazini pia yanahimiza raia kukaa mbali na ngome zinazoshikiliwa na wanajeshi - FAMA - na Wagner.

Vita vya mawasiliano vinaendeshwa na serikali ya Mali, ambayo wanaituhumu kwa kuendesha kwa maksudi na makundi ya kigaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.