Pata taarifa kuu

Mali :Raia 49 na wanajeshi 15 wauwawa katika shambulio wa wanajihadi.

Nairobi – Raia 49 na wanajeshi 15 wameuwawa nchini Mali jana usiku  baada ya shambulio la boti linalohusishwa na wanamgambo wa kislamu.

Wanajeshi zaidi ya 49 wameuwawa katika shambulio la wanajihadi
Wanajeshi zaidi ya 49 wameuwawa katika shambulio la wanajihadi © @Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa ni kuwa boti hilo lilishambuliwa lilipokuwa likisafiri kutoka Gao na  kunao raia waliojeruhiwa vibaya na huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Washambuliaji hao pia walivamia kambi ya kijeshi katika eneo la Bourem Circle, lililoko katika jimbo la Gao, kaskazini mashariki mwa Mali. Takriban washambuliaji 50 waliuawa katika makabiliano, na siku tatu za maombolezo ya kitaifa zilitangazwa, ilisema serikali ya mpito.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limekuwa likipambana na vuguvugu la wanajihadi lenye mafungamano na  lile la Al-Qaeda na kundi la Islamic State kwa takriban muongo mmoja.

Wanajihadi na wapiganaji wanaotaka kujitenga baadhi wakiwa na mfungamano na Al-Qaeda na kundi la Islamic State  walianza operesheni nchini Mali mwaka 2012 na mzozo huo umeenea hadi nchi jirani za Niger na Burkina Faso, na kuua na kuwafukuza maelfu ya raia.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya utawala wa kijeshi wa Bamako na nchi ya ufaransa umezorota katika miaka ya hivi karibuni huku jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi ikiweka vikwazo vikali kwa serikali ya Mali kuchelewa kurejea katika utawala wa kiraia.

Haya yanajiri wakati huu nchi jirani ya Niger and Gabon pia zikitawaliwa na jeshi.Kumbuka kuwa nchi hizi zote ni koloni ya Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.