Pata taarifa kuu

Mabilioni yaahidiwa kwa bara la Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

NAIROBI – Wakuu wa nchi mbalimbali barani Afrika na viongozi wa taasisi mbalimbali za Kimataifa, wamekuwa wakihutubia katika kongamano la Mazingira kuhusu bara la Afrika, ambalo linatamatika hivi leo jijini Nairobi nchini Kenya.

Katibu mkuu wa UN akitoa hotuba yake katika kongamano la Afrika la hali ya hewa 2023, jijini Nairobi, Kenya mnamo Septemba 5, 2023.
Katibu mkuu wa UN akitoa hotuba yake katika kongamano la Afrika la hali ya hewa 2023, jijini Nairobi, Kenya mnamo Septemba 5, 2023. AFP - LUIS TATO
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Falme za Kiarabu itakayokuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP 28 mwezi Novemba, imeahidi kutoa Dola Bilioni 4.5 ili kufadhili miradi ya kuzalisha nishati safi barani Afrika, kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Tutatoa dola bilioni 4.5 za Marekani ambazo zitachangia katika dola bilioni 12.5 za ziada kutoka kwenye vyanzo vya kimataifa vya umma na kibinafsi. Ni matarajio yentu kwamba hatua hii itaanzisha upya ushirikiano wa mageuzi na kuzindua matumaini ya kuinua mradi wa nishati safi kati bara hili muhimu. Amsema Sultan Al Jaber, Mkuu wa kampuni ya taifa ya mafuta ya Falme za Kiarabu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres naye amepata fursa ya kuhotubia mkutano huo, na kuyataka mataifa tajiri duniani, kutimiza ahadi yao ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kulisaidia bara la Afrika, kukumbatia nishati jadidifu.

Wajumbe wakitembea nje ya jumba la Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Kenya, Jumanne Septemba 5, 2023, wakati wa Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika.
Wajumbe wakitembea nje ya jumba la Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Kenya, Jumanne Septemba 5, 2023, wakati wa Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika. AP - Brian Inganga

Baraka Machumu, mtaalam wa nishati na mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania, anasema, licha ya mataifa ya Afrika kukabiliwa changamoto, kuna fursa za kuanza kutumia nishati hiyo.

Tunazo fursa nyingi kwenye upande wa nishati jadidifu, tunao upepo, tunao jua, na wataalam wapo lakini je kama taifa tuko tayari kuwatumia wale wataalam wapo wadogo kuhakikisha tunaanza vitu ambavyo ni vidogo vidogo 

Machumu amefafanua zaidi kuhusu mataifa ya Afrika kuanza kutumia nishati safi, akisema Afrika bado haijajijenga na lazima iwe na sauti moja kuhakikisha nchi za magharibi zinasikia kilio chao na kuwapa teknolojia kwa gharama nafuu kabisa.

Naye Samson Maanu, kutoka kampuni ya Suni Smart energy inayokuza mapato ya kaboni, anagusia ukosefu wa ufadhili unavyorudisha nyuma matumizi ya nishati jadidifu.

Tuko na raslimali hizo zote lakini changamoto kubwa ni vile watu wanapata ufadhili wa kufanikisha hii miradi.

Kuelekea tamati ya kongamano hili siku ya jumatano, sekta na nishati ni miongoni mwa zinazotakiwa kutafutiwa ufumbuzi, ili Afrika iachane na nishati inayochagua mazingira.

Wajumbe wanaohudhuria mkutano huo, wanatarajiwa kuja na msimamo wa pamoja kuhusu namna ya kulisaidia bara la Afrika linalokabiliana na ukame lakini pia mafuriko, kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Ripoti yake mwandishi wetu Minzilet Ijai, Nairobi, Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.