Pata taarifa kuu

Operesheni Shujaa kuendelea mashariki mwa DRC kwa miezi 4 zaidi

NAIROBI – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jeshi la FARDC na lile la Uganda UPDF wamekubaliana kuendelea na operesheni Shujaa kwa miezi minne zaidi, kukabiliana na waasi wa ADF Mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Museveni alikutana na maafisa wakuu wa jeshi la Uganda (UPDF) na Jeshi la Kongo (FARDC) katika Ikulu ya Entebbe ili kukagua maendeleo ya Operesheni Shujaa nchini DRC mnamo Agosti 30, 2023.
Rais Museveni alikutana na maafisa wakuu wa jeshi la Uganda (UPDF) na Jeshi la Kongo (FARDC) katika Ikulu ya Entebbe ili kukagua maendeleo ya Operesheni Shujaa nchini DRC mnamo Agosti 30, 2023. © @StateHouseUg
Matangazo ya kibiashara

Akida wa majeshi ya Uganda jenerali Wilson Bandi na mwenzie wa Kongo jenerali Christian TSHIWEWE, wamekubaliana hilo katika mkutano wa Kampala, wenye lengo la kukagua na kutathmini maendeleo ya operesheni Shujaa.

Duru za FARDC-UPDF zinakadiria zaidi ya waasi 500 wameuawa tangu kuanza kwa operesheni hiyo mnamo Novemba 30, 2021.

Kwa mujibu wa wanaharakati, mauaji ya Raia yanayotekelezwa na waasi wanaodhaniwa kuwa ni ADF na washirika wao, yamepungua kwa asilimia 90 mashariki mwa Beni na Ituri.

Kanali Deo Akiiki ambaye ni makamu msemaji wa operesheni Shujaa amezungumzia operesheni hii akisema ifikapo mwezi Disemba watarejea kufanya tathmini zaidi.

Kingine muhimu ni kwamba operesheni hiyo imepata matunda ambayo inajulikana, wananchi wamerudi nyumbani kwa sehemu za Muhalika, Ruwenzori, Irumu. Sasa hivi adui amekimbia huko sehemu za Mambasa  na tunategemea kwamba operesheni hizi zitaendelea mpaka adui tutamtafuta sehemu zozote ambayo atajificha.

Mapendekezo ya raia mashariki mwa Kongo ni operesheni Shujaa kuelekea magharibi ya Beni, Irumu na Mambasa, kama vile baadhi yao wamezungumza.

Hali ya usalama inaendelea kuwa mbovu sana katika maeneo ya magharibi na barabara taifa 4, ADF wanaua watu kila siku kuna hata watu ambao hawa jazikwa"  amesema raia mmoja.

Raia mwingine katika eneo hilo amependekeza operesheni hiypo kuendelea hadi barabara kutoka Eringeti kuelekea Kamanda, akisema hatua hiyo itaweza kupunguza ukali wa adui.

Eriksson LUHEMBWE Beni Rfi kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.