Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC na Burundi zatia saini makubaliano ya ulinzi na usalama

Burundi na DRC zimehitimisha, Jumatatu hii, Agosti 28 katika ukumbi wa Palais de la Nation mjini Kinshasa, mkataba wa maelewano baina ya nchi mbili kuhusu ulinzi na usalama. Lengo lililotajwa ni kuimarisha usalama katika nchi hizo mbili.

Mkutano na waandishi wa habari wa Marais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi, Agosti 28 katika Palais de la Nation huko Kinshasa.
Mkutano na waandishi wa habari wa Marais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi, Agosti 28 katika Palais de la Nation huko Kinshasa. © Photo presidence de la République
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo ulitiwa saini na Alain Tribert Mutabazi, Waziri wa Ulinzi wa Burundi na yule wa DRC, Jean-Pierre Bemba.

Hafla hiyo imefanyika mbele ya Marais Evariste Ndayishimiye na Félix Tshisekedi.

Muda mfupi kabla, marais wa Burundi na mwenzake wa Kongo walijadili masuala ya miundombinu, biashara na mengine. Kisha wakafanya mkutano na waandishi wa habari.

Mkataba wa kijeshi ambao Burundi inasaini na DRC hauna nia ya kuingilia ujumbe unaoongozwa na Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC), amesema Ndayishimiye.

Kwake, "DRC na Burundi ni kama gome na mti na kwa hivyo lazima zihifadhi masilahi yao kwa njia ya pamoja".

Katika sekta ya kibiashara, Wakuu hao wawili wa Nchi wamekubaliana juu ya haja ya kuunda matawi ya benki za Burundi na Kongo huko Bukavu na Uvira, nchini DRC na pia Bujumbura na Rumonge, nchini Burundi. Hii, ili kurahisisha shughuli kati ya nchi zao.

Sambamba na hilo, wametaka kuimarishwa kwa kubadilishana uzoefu na utaalamu kati ya wizara za kisekta katika nyanja za kilimo na miundombinu na viwanda.

Kuhusu vita vya M23

Katika mkutano huu na waandishi wa habari, marais hao wawili pia walijadili suala la vita vilivyoanzishwa na M23 mashariki mwa DRC na majibu ya kanda , hususan EAC, kukomesha.

Kwa mjibu wa Felix Tshisekedi, "mahitaji ya DRC yanasalia kuwa yale yale, tunaomba kwamba jeshi la kikanda lifanye kazi zaidi kama kikosi cha Burundi kwa sababu katika baadhi ya maeneo, kuna ulegevu fulani".

Rais wa sasa wa EAC na Mkuu wa Nchi wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, kwa upande wake, alikumbusha kuwa "Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki imejizatiti katika dhamira yake ya kukomesha uwepo wa makundi yenye silaha na zaidi kuleta M23." waasi kufuata maagizo ya mchakato wa Nairobi.

Katika taarifa ya mwisho, Evariste Ndayishimiye na Felix Tshisekedi "walibainisha na kusikitishwa na ukweli kwamba M23 hawana nia ya kujiondoa na kwenda kwenye kambi walikotakiwa kukusanyika".

Kwa ajili hiyo, inaongeza taarifa hii kwa vyombo vya habari, "wamezindua wito kwa kanda kuchukua majukumu yake ya kuwalazimisha M23 kwenda kwenye kambi walikotakiwa kukusanyika".

Hivyo Rais Evariste amemaliza ziara yake ya saa 48 mjini Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.