Pata taarifa kuu

Niger: Utawala wa kijeshi waamuru kuondoka kwa balozi wa Ufaransa

Wanajeshi walio madarakani nchini Niger tangu mapinduzi ya Julai 26 wameamuru, Ijumaa hii Agosti 25 kwa taarifa kwa vyombo vya habari, kuondoka kwa balozi wa Ufaransa nchini Niamey, Sylvain Itté. Balozi huyu ana saa 48 kuondoka nchini Mali, imesema Wizara ya Mambo ya Kigeni ya serikali iliyoundwa na wanajeshi.

Waandamanaji wakiwa na bango lililoandikwa "Ufaransa lazima iondoke" wakati wa maandamano ya siku ya uhuru huko Niamey mnamo Agosti 3, 2023.
Waandamanaji wakiwa na bango lililoandikwa "Ufaransa lazima iondoke" wakati wa maandamano ya siku ya uhuru huko Niamey mnamo Agosti 3, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na "kukataa kwa balozi wa Ufaransa huko Niamey kujibu mwaliko" wa wizara "kwa mahojiano" siku ya Ijumaa "na hatua zingine za serikali ya Ufaransa kinyume na masilahi ya Niger", viongozi "wameamua kumtaka Bw. Sylvain Itté kuondoka mara moja nchini Niger na kumtaka kuondoka kwenye ardhi ya Niger ndani ya saa arobaini na nane", inaonyesha taarifa kwa vyombo vya habari.

Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa haikupatikana mara moja kuzungumzia hatua hiyo.

tangu mapinduzi ya kijeshi Julai 26, uhusiano kati ya Niger na Ufaransa umedorora kwa kiasi kikubwa. Ufanransa unaunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba nchini iger na rais aliyetimuliwa mamlakani Bw. Bazoum aachiliwe na arejeshwe mamlakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.