Pata taarifa kuu

KInshasa yafutilia mbali shutma za HRW kuhusu dhulma zinazofanywa dhidi ya upinzani

Mamlaka ya DRC siku ya Alhamisi imekanusha mashtaka ya "ukandamizaji" na "kutishia" wapinzani yaliyotolewa dhidi yake na sjhirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch kabla ya uchaguzi wa urais katika nchi hii ambapo wanaharakati kumi na wawili wanaounga mkono demokrasia wamekamatwa huko mashariki, kulingana na mashirika yao.

Vikosi vya usalama vinashika doria katika mitaa ya Kinshasa baada ya makabiliano kati ya polisi na waandamanaji wa upinzani Mei 20, 2023.
Vikosi vya usalama vinashika doria katika mitaa ya Kinshasa baada ya makabiliano kati ya polisi na waandamanaji wa upinzani Mei 20, 2023. © Justin Makangara/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne Human Rights Watch (HRW) ilishutumu, katika ripoti yake, "ukandamizaji" na "vitisho" vinavyokabili upinzani wa kisiasa, miezi minne kabla ya uchaguzi wa urais, "katika muktadha wa mvutano mkubwa wa kisiasa". Ikirejelea "visa vya watu kukamatwa na kuzuiwa kwa uhuru wa kimsingi", shirika hili la haki za binadamu lilisema kuwa mamlaka ya DRC "imewalenga viongozi wa vyama vya kisiasa".

"DRC inafutilia mbali madai ya kuvunjwa kwa uhuru wa kimsingi, watu kukamatwa kiholela na vitisho",imejibu Kinshasa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Mawasiliano.

Hali ya kisiasa ni ya wasiwasi nchini DRC ambapo uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika Desemba 20. Uchaguzi huo utaambatanishwa na uchaguzi wa wabunge wa kitaifa na wa magavana. Upinzani unaishutumu serikali kwa kutaka kuandaa "chaguzi zenye machafuko". Serikali inashutumu "mkakati wa sehemu ya upinzani unaojumuisha kudharau mchakato wa uchaguzi", imeandikwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Huko Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini (mashariki), wanamgambo kumi na wawili wa vuguvugu la LUCHA "wamekamatwa kikatili" karibu na mitambo ya tume ya uchaguzi "waliposhutumu utaratibu wa ugawaji wa nakala kwa wale ambao walikuwa na kadi zisizosomeka,” amesema kiongozi wa vuguvugu hilo Bienvenu Matumo.

Bw. Matumo anaomba “waachiliwe mara moja”. Lucha iliyoanzishwa mnamo mwaka wa 2012 huko Goma, linawaleta pamoja vijana "weye hasira" na kudai kuwa hawaegemei upande wowote katika siasa, na waendesha harakati zao kwa amani, lakini wamedhamiria kuwawajibisha viongozi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.