Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

HRW yalaani 'ukandamizaji' na 'vitisho' dhidi ya upinzani nchini DRC

Miezi minne kabla ya uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch siku ya Jumanne limeshutumu 'ukandamizaji' na 'vitisho' vinavyokabili upinzani wa kisiasa, "katika muktadha wa mvutano mkubwa wa kisiasa".

Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Chérubin Okende, hapa ilikuwa mwezi Machi 2023, alipatikana amekufa mnamo Julai 13, 2013, mwili wake ukiwa majeraha ya risasi.
Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC Chérubin Okende, hapa ilikuwa mwezi Machi 2023, alipatikana amekufa mnamo Julai 13, 2013, mwili wake ukiwa majeraha ya risasi. AP - Samy Ntumba Shambuyi
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya DRC "imewalenga viongozi wa vyama vya kisiasa" kulingana na shirika la haki za binadamu la Marekani. Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumanne, HRW inazungumzia "watu wengi kukamatwa na kuvunjwa kwa uhuru wa kimsingi".

Ikinukuliwa na Human Rights Watch, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini DRC inarejelea "utekaji nyara na vitisho vinavyolenga upinzani", "matamshi ya chuki na uchochezi wa ghasia", pamoja na "matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wa amani".

Matukio mengi yaliyoripotiwa katika waraka huu yanahusu chama cha Ensemble pour la République cha Moïse Katumbi, mtu maarufu katika siasa za Kongo, ambaye  ni mmoja wa wapinzani wakuu wa utawala wa Rais Félix Tshisekedi.

Mnamo Mei 30, mshauri wa kwanza wa Bw. Katumbi, Salomon Kalonda, alikamatwa mjini Kinshasa na maafisa wa ujasusi wa kijeshi na bado anazuiliwa hadi leo. Mashtaka dhidi yake yamebadilika mara kadhaa tangu kukamatwa kwake.

Mnamo tarehe 13 Julai, Chérubin Okende, msemaji wa Ensemble pour la République, alipatikana amekufa, baada ya kupigwa risasi katika gari lake, kando ya barabara katika mji mkuu Kinshasa.

Waziri huyu wa zamani wa Uchukuzi wa Felix Tshisekedi alijiunga na Moïse Katumbi na upinzani mwishoni mwa mwaka 2022. "Mauaji" yake, ambayo hadi sasa hayajashughulikiwa, yalisababisha mtafaruku kote nchini.

Mnamo Mei 24, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Waziri mpya wa Mambo ya Ndani aliyeteuliwa hivi karibuni Peter Kazadi aliwashambulia waandishi wa habari wa kimataifa na jumuiya ya kimataifa kujibu ukosoaji wa ukandamizaji mkali dhidi ya maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.