Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mzozo wa kikabila magharibi mwa DRC: Takriban watu 300 wameuawa tangu mwezi Juni

Ghasia za kijamii zinazoendelea magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimesababisa watu 300 kupoteza maisha tangu mwezi Juni 2022, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema katika ripoti iliyotolewa leo Alhamisi.

Baada ya mvua, wafanyabiashara wanaondoka sokoni na mizigo yao huko Kitshanga, kilomita 90 kutoka mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo Desemba 10, 2022.
Baada ya mvua, wafanyabiashara wanaondoka sokoni na mizigo yao huko Kitshanga, kilomita 90 kutoka mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo Desemba 10, 2022. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi Oktoba, serikali ya DRC ilikadiria 'zaidi ya watu 180' idadi ya waliofariki katika mzozo huu kati ya jamii za Teke na Yaka. Kisha ailibaini kuwa hali "imedhibitiwa", lakini mzozo ulioanzia katika mkoa wa Maï-Ndombe na kuenea hadi mkoa jirani wa Kwilu, umeendelea na vurugu zinaendelea.

Machafuko hayo yalimesababisha "angalau vifo 300 wakati wa mashambulizi na ulipizaji kisasi", linaandika shirika la Human Rights Watch. "Serikali inapaswa kushughulikia kwa haraka mizozo ya muda mrefu kuhusu mamlaka ya kimila na haki za ardhi ili kuzuia kutokea tena kwa ghasia hizo," shirika la haki za binadamu limeiongeza.

Vurugu hizo zilianzia kwenye mgogoro wa ardhi kati ya Wateke wanaojinasibu kuwa ni wazawa na wamiliki wa vijiji vilivyopo kando ya mto Kongo umbali wa takribani kilomita 200 na Wayaka waliokuja kuishi baada yao.

"Wanakijiji kutoka jamii zenye watu wengi za Teke na Yaka, wote walijiingiza katika mzozo wa malipo ya ardhi na upatikanaji wa ardhi, waliharibu, kuporwa na kuchoma mamia ya nyumba pamoja na shule na vituo vya afya," linasema HRW. Shirika hili linaongeza kuwa "kuanzia mwishoni mwa mwezi Juni, watu kutoka jamii ya Yaka walijipanga katika vikundi, vilivyoitwa 'Mobondo' ikimaanisha miungu".

"Wakiwa na mapanga, visu, mikuki, pinde na mishale, bunduki kuwinda na bunduki chache za kijeshi, waliwashambulia na kuwaua makumi ya wanakijiji wa Teke, kulingana na mashahidi wengi," ripoti hiyo yasema. "Baadhi ya wanakijiji wa Teke walishiriki katika mlipuko wa awali wa vurugu, wakilenga Yaka na maduka na nyumba zao," HRW pia inaandika. "Hata hivyo, washambuliaji wa Mobondo walichukua madaraka haraka," kulingana na shirika hilo.

HRW iliongeza kuwa "serikali haikuimarisha nguvu kazi ya vikosi vya usalama vya mkoa, hata hivyo ilizidiwa, kabla ya mwezi Septemba, na haikutoa msaada wa kutosha kwa zaidi ya watu 50,000 waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia". Kulingana na shirika hilo lisilo la kiserikali, baadhi ya maafisa wa vikosi vya usalama vya Kongo wenyewe "walifanya mauaji, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kikatili, uporaji na unyanyasaji wa kingono".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.