Pata taarifa kuu

Zimbabwe: Mgogoro mkali wa kiuchumi na mfumuko wa bei sugu kuelekea uchaguzi mkuu

Kulingana na kura ya maoni ya hivi majuzi, uchumi na ukosefu wa ajira ndio wasiwasi kubwa ya wapiga kura. Kwa sababu nchi hii inakabiliwa na muktadha wa mgogoro mkubwa wa kiuchumi. 

Zoezi la upigaji kura mjini Harare, kwa uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe, Julai 30, 2018.
Zoezi la upigaji kura mjini Harare, kwa uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe, Julai 30, 2018. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa matatizo mengine, uchumi wa Zimbabwe unakabiliwa na mfumuko wa bei wa kudumu. Baada ya kuongezeka mnamo 2020, mfumuko wa bei ulipungua mnamo mwezi Julai, lakini bado unazidi 100%: baadhi ya wachumi wanakadiria kuwa juu zaidi kuliko takwimu rasmi.

Lakini shida zingine za kimuundo zinapaswa kuzingatiwa. “Takriban 90% ya Wazimbabwe wameajiriwa kwa njia isiyo rasmi. Na karibu asilimia 42 ya watu wanaishi katika umaskini uliokithiri,” anasema Prosper Chitambara, mwanauchumi wa maendeleo mjini Harare.

Zimbabwe ambayo ni hifadhi ya zamani ya nafaka kwa ukanda huo, iimejikuta uzalishaji wake wa kilimo ukishuka baada ya mageuzi ya ardhi ya miaka ya 2000. Baada ya mwaka 2008, ukuaji uliongezeka lakini majanga mengine yalitikisa uchumi wa nchi hii.

Prosper Chitambara anataja hali ya hewa, janga la UVIKO-19 na vita nchini Ukraine. Aidha, mazingira hayafai kwa uwekezaji: “Upatikanaji wa mikopo ni mgumu na ni ghali sana. Kiwango cha riba cha marejeleo ni 150%. "

Miradi ya miundombinu yenye mikopo ya China

Prosper Chitambara hata hivyo anakaribisha baadhi ya mambo chanya kwa uchumi: “Tumeona idadi fulani ya uwekezaji katika miradi ya miundombinu, kama vile barabara kuu, mabwawa na ongezeko la uzalishaji wa umeme. "

Miradi minne ya nishati imefanywa kwa mkopo kutoka China. Inadaiwa, Zimbabwe haistahiki ufadhili kutoka kwa wafadhili wa kimataifa, kama vile IMF na Benki ya Dunia... kwa sababu ya malimbikizo.

Mbali na vikwazo vya Magharibi kwa tuhuma za ufisadi, Harare pia inalengwa na vikwazo kwa ukiukaji wa haki.

Hatari ya ghasia za uchaguzi ni ndogo, wachambuzi wanasema. Wanatabiri idadi ndogo ya wapiga kura baada ya kampeni iliyovutia wapiga kura wachache.

Kwa sababu kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Ringisai Chikohomero, chaguzi hizi zinafanyika wakati "hakuna shauku yoyote na ni jambo lisilo la kawaida wakati wa kipindi cha uchaguzi", hasa kutokana na "hali ya vitisho" inayowasukuma "Wazimbabwe kujikagua kwa hofu za kulipiza kisasi".

Chaguzi hizi zinafanyika katika muktadha tofauti kabisa na ule wa awali wa mwak 2018: ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Wazimbabwe kufanya uchaguzi bila ya kuwepo kwa Robert Mugabe.

Sasa kuna uchovu wa wapiga kura, kwani matumaini ya mabadiliko baada ya Robert Mugabe kuwa madarakani kwa takriban miaka 30 yamefifia haraka: Bunge limepitisha sheria ambazo, kulingana na mashirika ya haki za binadamu, zinaziba mdomo mashirika ya kiraia na kupunguza ukosoaji wowote wa serikali. Na miongoni mwa wapiga kura, kuna uchovu fulani, anaeleza Ringisai Chikohomero.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.