Pata taarifa kuu

Uchaguzi Zimbabwe: Mfahamu Mchungaji 'kijana' Nelson Chamisa

Mwanaharakati kwa miongo kadhaa, kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe na anayedai kuwa katika ofisi kuu Nelson Chamisa, mwanasheria na mchungaji wa miaka 45, bado anajiita "kijana".

Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari.katika hoteli ya Bronte Hotel huko Harare, on August 3, 2018
Kiongozi wa upinzaji nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari.katika hoteli ya Bronte Hotel huko Harare, on August 3, 2018 AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Jina hili la utani linasisitiza tofauti yake ya umri na rais anaye maluza muda wake Emmerson Mnangagwa, 80, anayejulikana kama "mamba" kwa ukatili wake, ambaye anakabiliana naye siku ya Jumatano katika uchaguzi wa urais. Pia inafanya jina lake lisiwezi kutamkwa hadharani, katika nchi ambayo Zanu-PF,chama kilicho madarakani tangu uhuru, kinajihusisha na ukandamizaji kwa miezi kadhaa bila kuchaguwa wapinzani.

Zimbabwe, yenye utajiri wa dhahabu na madini, iko chini ya utawala wa 'kiimla', mkuu wa Muungano wa Mabadiliko ya Wananchi (CCC) Nelson Chamisa aliliambia shirika la habari la AFP mapema mwaka huu. Nafasi yake ya kushinda inaonekana kuwa ndogo. Mikutano ya "Triple C" imepigwa marufuku, baadhi ya maafisa wake waliochaguliwa kukamatwa na kutupwa jela, na hofu ya wizi wa kura imeenea.

Chamisa analijua hilo. Nelson Chamisa, alikamatwa mara kadhaa kwa shughuli zake za kisiasa. Mnamo 2007, alipigwa kwa chuma na kuachwa akidhaniwa amekufa, shambulio lililohusishwa na majambazi kutoka chama tawala. Mnamo 2021, aliepuka kile anachoelezea kama jaribio la mauaji wakati msafara wake ulishambuliwa kwa risasi. Risasi ilipitia kiti cha nyuma cha kushoto cha gari lake, mahali anapokaa kawaida. "Nina bahati ya kuwa hai," amesema.

Akiwa mwanafunzi, alijiunga na chama cha Movement for Democratic Change (MDC) kilipoanzishwa mwaka wa 1999. Alikiongoza baada ya kifo cha mtangulizi wake, Morgan Tsvangirai, mwaka wa 2018. Mwaka huohuo, Chamisa nusura ampige mweleka Mnangagwa katika uchaguzi wa urais.Uchaguzi uliokuwa wa ushindai, wa kwanza kufanyika baada ya Robert Mugabe kuondolewa madarakani. Alipinga matokeo lakini alishindwa mahakamani. Ghasia zilizuka, waandamanaji sita waliuawa na jeshi.

Mnamo 2022, Chamisa alikihama chama cha MDC na kuunda chama chake, ambacho rangi yake ni ya manjano, kikiwa na nia ya kujaribu bahati yake tena. Wapiga kura waliotishwa na hali mbaya ya uchumi wa Zimbabwe, ufisadi na mfumuko wa bei uliokithiri, walijiunga naye lakini alikosolewa, ikiwa ni pamoja na ukosoaji kutoka kambi yake mwenyewe.

Maono yasiyo sahihi

"Pia ana uhakika sana juu yake mwenyewe, pengine kimakosa," amesema Nicole Beardsworth, mwanachuoni wa Afrika Kusini. Mtindo wake wa uongozi unainyima CCC miundo, pia kwa hofu ya kuingiliwa na mamlaka iliyopo. Wakosoaji wake wanaamini kuwa amekidhoofisha chama, na kuleta mkanganyiko na kutojipanga wakati uchaguzi unakaribia.

CCC inawasilisha wagombea katika baadhi ya maeneo ya uchaguzi, haina wagombea katika maeneo mengine. Pia anatatizika kujieleza katika maeneo ya mashambani, wakosoaji wake wakimtuhumu kwa kutofanya kampeni ya kuridhisha ya usajili wa wapiga kura wapya. Wengine pia wanamkosoa kwa kutofaulu kutangaza programu, sera kwa nchi.

Mungu na dini hujitokeza sana katika jumbe za Chamisa, zikiwatenga baadhi ya wapiga kura wa mijini. Mzaliwa wa Masvingo, kusini mwa mji mkuu wa Harare, Chamisa alisomea sheria, sayansi ya siasa na teolojia. Anahusisha taaluma yake kwa msaada wa wazazi wake kwamba alifaulu shuleni.

Akiwa mkuu wa chama kikuu cha wanafunzi mwishoni mwa miaka ya 1990, alikuwa mmoja wa waandalizi wa maandamano dhidi ya serikali ya Mugabe. Alipanda ngazi kupitia MDC, na kuwa kiongozi wa vuguvugu la vijana na msemaji wake. Alikuza urahisi wake katika kuzungumza hadharani, aliandika hotuba zenye hisia kali zilizochoshwa na ucheshi, ambazo ni tofauti na Mnangagwa.

Katika serikali ya kugawana madaraka iliyoanzishwa mwaka 2008, alikua waziri mwenye umri mdogo zaidi, anayesimamia habari. "Chamisa ni mkarimu sana", anasisitiza mwaachuoni kutoka Zimbabwe Brian Raftopoulos, ambaye anataja, kati ya "udhaifu wake", "kutokuwa na uwezo wa kuwajibika ndani ya chama chake" na "ukosefu wa maono ya muda mrefu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.