Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-USALAMA

Zimbabwe: Mahakama Kuu yakataa kutoa nafasi kwa upinzani kufikia daftari la wapiga kura

Tarehe 23 Agosti, zaidi ya wapiga kura milioni 6 wa Zimbabwe wataitwa kupiga kura kumchagua rais wao mpya na wabunge katika mazingira ya mvutano. Rais anayeondoka madarakani, Emmerson Mnangagwa, ambaye alimpindua Robert Mugabe mwaka 2017, ananuia kushikilia nafasi yake. Hata hivyo, upinzani umekuwa ukikabiliwa na marufuku ya mikusanyiko na wafuasi wake kukamatwa kwa miezi kadhaa. Daftari la wapiga kura ni jambo nyeti, ambalo limesumbua chaguzi zilizopita.

Kiongozi wa muungano wa Wananchi kwa ajili ya Mabadiliko (CCC), Nelson Chamisa, akizungumza na wafuasi wake wakati wa mkutano katika viunga vya Harare, Julai 26, 2023.
Kiongozi wa muungano wa Wananchi kwa ajili ya Mabadiliko (CCC), Nelson Chamisa, akizungumza na wafuasi wake wakati wa mkutano katika viunga vya Harare, Julai 26, 2023. AP - Tsvangirayi Mukwazhi
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kanda hiyo, Claire Bargelès

Wiki hii, Mahakama Kuu ya Harare ilikataa kuupa nafasi muungano wa Wananchi kwa ajili ya Mabadiliko (CCC), chama cha upinzani cha Nelson Chamisa, kupata toleo jipya la daftari la wapiga kura. Jaji anaona kuwa hili ni ombi "lisilo la dharura", ingawa uchaguzi utafanyika chini ya wiki moja. Mapema mwaka huu, mahakama ilikataa ombi la kuchapishwa kwa toleo la kielektroniki la daftari la wapiga kura, ikizingatiwa kuwa ni "hati nyeti".

Chama kikuu cha upinzani kinashutumu ukiukaji wa Katiba na kuhofia kuwa orodha hiyo itabadilishwa ili kuvuruga uchaguzi. Wakati toleo la kwanza la daftari la wapiga kura lilipopatikana, watu wengi walishangaa kutoona majina yao kwenye daftari hilo, huku wengine wakijikuta wamehamishwa hadi vituo vya mbali zaidi vya kupigia kura.

Wanaharakati kutoka chama cha Team Pachedu pia wanakashifu makosa mengi, kwa mfano, nambari za utambulisho zilizoambatishwa kwa majina tofauti ikilinganishwa na faili za awali. Sintofahamu ya kiutawala, au mkakati halisi: kwa mujibu wa shirika la Human Rights Watch, hii kwa vyovyote ni mojawapo ya sababu kwamba mazingira ya uchaguzi huu hayawezi kuchukuliwa kuwa "ya kuaminika, huru na ya haki".

CCC inaendelea kutumia taratibu zote za kisheria ili kujaribu kupata toleo hili la mwisho la daftari la wapiga. Chama hicho pia kinashutumu kasoro nyingi katika upigaji kura wa maafisa wa polisi kupitia posta, ambao ulianza wiki hii, na kinadai kupokea ushuhuda kutoka kwa maafisa waliolazimishwa kupiga kura mbele ya wakuu wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.