Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Wapinzani arobaini wa Zimbabwe wakamatwa wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais

Siku ya Jumanne nchini Zimbabwe, wapinzani arobaini walikamatwa wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge, wakati wa gwaride la kampeni katika kitongoji cha mji mkuu Harare, kulingana na chama kikuu cha upinzani na polisi.

Polisi imethibitisha katika taarifa kukamatwa kwa "wanaharakati 40 wa CCC" kwa kukiuka utaratibu wa umma. Kulingana na polisi, wapinzani hawakuheshimu eneo lililotangazwa kwa mamlaka kwa operesheni ya kampeni.
Polisi imethibitisha katika taarifa kukamatwa kwa "wanaharakati 40 wa CCC" kwa kukiuka utaratibu wa umma. Kulingana na polisi, wapinzani hawakuheshimu eneo lililotangazwa kwa mamlaka kwa operesheni ya kampeni. AFP
Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inafanya Uchaguzi Mkuu Agosti 23, katika hali ya mvutano. Rais Emmerson Mnangagwa, ambaye anawania kiti cha urais, amekuwa akishutumiwa kwa miezi kadhaa na upinzani kwa kuendesha ukandamizaji unaoongezeka.

Wanachama 40 wa Muungano wa Mabadiliko ya Wananchi (CCC) "walikamatwa walipokuwa wakishuka barabarani kwa maandamano," msemaji wa CCC Fadzayi Mahere ameliambia shirika la habari la AFP. Baadhi walisimama nyuma ya lori, wengine waliandamana kwa miguu, kulingana na picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Polisi imethibitisha katika taarifa kukamatwa kwa "wanaharakati 40 wa CCC" kwa kukiuka utaratibu wa umma. Kulingana na polisi, wapinzani hawakuheshimu eneo lililotangazwa kwa mamlaka kwa operesheni ya kampeni.

Katika uchaguzi huo utakaofanyika wiki ijayo, Bw Mnangagwa, 80, atapambana na Nelson Chamisa, wakili na mchungaji mwenye umri wa miaka 45, ambaye anaongoza CCC. Muungano huo wiki jana ulishutumu "vurugu za kisiasa" wakati uchaguzi ukikaribia, lakini Bw. Chamisa aliapa hatakata tamaa.

Mwaka wa 2017 Bw. Mnangagwa alichukuwa mikoba ya Robert Mugabe, shujaa wa uhuru aliyetawala nchi hiyo kwa miaka 37, kutokana na mapinduzi ya kijeshi. Alichaguliwa kuwa rais mwaka uliofuata, akishinda kwa kiasi kidogo (50.8%) baada ya uchaguzi uliyokubwa na vurugu.

Nchi hiyo isiyo na bahari imekuwa ikitawaliwa na chama kimoja tangu uhuru wake mwaka 1980 na tuhuma za ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi huripotiwa mara kwa mara nchini humo. Katika ripoti ya hivi majuzi, Human Rights Watch ilishutumu "mchakato wa uchaguzi wenye upendeleo mkubwa" kabla ya uchaguzi ujao. Shirika hilo lilishutumu polisi kwa kuwa "washiriki" na kutumia "vitisho na vurugu dhidi ya upinzani".

Zimbabwe ambayo inakabiliwa na umaskini, mfumuko wa bei na ukosefu wa ajira uliokithiri, imekuwa ikikumbwa na matatizo makubwa ya kiuchumi kwa miaka ishirini iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.