Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Rais wa Zimbabwe aahidi uchaguzi wa urais kuwa 'huru na wa haki'

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, anayeshutumiwa kwa kuongeza kasi ya kukandamiza sauti zinazompinga kabla ya uchaguzi wa urais mwaka huu, aliahidi siku ya Jumanne kwamba uchaguzi utakuwa 'huru na wa haki'.

Serikali ya Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa imekanusha kuwepo kwa mgogoro wowote.
Serikali ya Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa imekanusha kuwepo kwa mgogoro wowote. AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmerson Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 80, ambaye atawania katika uchaguzi huo wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti lakini tarehe yake bado haijathibitishwa, katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 43 ya uhuru wa taifa hilo, alitoa wito wa 'kutojihusisha na vurugu, kabla, wakati na baada ya uchaguzi'.

Serikali yangu imechukua hatua kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika," alisema katika mji mdogo wa Mlima Darwin yapata kilomita 155 kaskazini mashariki mwa mji mkuu Harare.

Historia ya kisiasa ya nchi hii ya kusini mwa Afrika inaangaziwa na vurugu na vitisho wakati wa uchaguzi. Akiingia madarakani mwaka wa 2017 katika mapinduzi dhidi ya gwiji mkuu wa nchi hiyo, Robert Mugabe, Bw. Mnangagwa alishinda uchaguzi wa urais mwaka uliofuata kwa asilimia 50.8 ya kura.

Chama cha mpinzani wake mkuu, Nelson Chamisa, 45, kinamtuhumu kwa kuwakandamiza wapinzani wa kisiasa. Katika wiki za hivi karibuni, mikutano ya upinzani imezuiwa na viongozi wakiwemo wabunge kukamatwa. Emmerson Mnangagwa ambaye ameshindwa licha ya ahadi za kurejesha uchumi unaodorora kwa miaka ishirini, anakabiliwa na hasira za wananchi.

Katika hotuba yake siku ya Jumanne, alionya dhidi ya "sauti, za kigeni au za ndani, ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali yasiyo ya uaminifu" ambayo "yanachochea migawanyiko na mifarakano". Bunge lilipitisha sheria yenye utata mapema mwezi Februari inayozuia kwa kiasi kikubwa uhuru wa mashirika yasiyo ya kiserikali, na kuyaweka chini ya udhibiti wa serikali na chini ya vikwazo vinavyowezekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.